beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Mbunge wa Kinondoni, Tarimba Gulam Abbas ameishauri Serikali kuangalia utaratibu mzuri wa kupanua wigo wa Walipakodi badala ya kuongeza Kima cha Kodi
Akichangia Mjadala wa Bajeti Kuu amesema, "Tatizo lililopo hasa upande wa Serikali, wanamlenga Mlipakodi wanayemuona. Leo iwe 10% kesho iwe 12% kama njia ya kupandisha Mapato"
Amesema utaratibu huo ni mbaya, akishauri Mamlaka kuweka Kima kidogo ili watu wengi waweze kulipa kodi. Amesema kuweka Kima kikubwa kutapelekea Watanzania kutafuta njia ya kupenya na kutolipa Kodi