Kada ya CCM Tarime mkoa wa Mara Zakayo Wangwe aelezea kwa kina hali ya siasa Tarime na changamoto iliyopo ikiwa mbunge wa CCM Waitara atapitishwa kugombea 2025
Kada Zakayo Wangwe amesema kuwa kuna makundi ya CCM Halisi na CCM wakuja ya Waitara yanayokinzana na kumlaunu mbunge Waitara ndiye muasisi wa mgawanyiko ndani ya CCM katika wilaya ya Tarime, hali inayopelekea tishio CCM chama dola kongwe kuweza kushindwa ubunge Tarime ...
Kada wa CCM ndugu Zakayo Wangwe amekwenda mbali na kuanika tabia ya Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara (CCM) alivyosababisha migogoro ndani ya CHADEMA kabla ya kutimkia CCM ....
Kada huyo wa CCM ndugu Zakayo Wangwe ameongeza kuwa kutokana na mgawanyiko aliouunda Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara (CCM), sasa makada na viongozi wa CCM Tarime wanaishi kwa hofu ya kutoaminiana, watumishi wa CCM kuhamishwa n.k hivyo chama dola kongwe kukosa umoja ndani ya chama cha mapinduzi ....
Kudhihirisha kuwa Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara (CCM) hakubaliki katika jamii ya Tarime, ni pale wananchi walipomzomea na kupiga yowe kitu ambacho kiongozi ktk jamii ya Tarime ni nadra kutokea kwa sababu ya heshima wanayowapa viongozi wao, lakini kwa Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara (CCM) wananchi uzalendo pamoja na mila za Tarime uliwashinda hivyo wakamzomea na kupiga yowe la kumkataa ....
Kada huyo ndugu Zakayo Wangwe ameomba mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dr. Samia Hassan na katibu mkuu wa CCM balozi Dr. Nchimbi watumie mamlaka zao na mfumo ndani ya chama kongwe dola kukinusuru chama cha CCM Tarime kilichotekwa nyara na kuendeshwa kijeshi chini ya mamluki wa Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara (CCM).
Waitara ametua ushawishi wake kuhakikisha chama kinaburuzwa bila demokrasia hivyo kuwepo mgawanyiko wa kisiasa ktk CCM Tarime .... mpasuko huo ambao wanaCCM wanasema utakinufaisha chama cha CHADEMA pakubwa kushinda chaguzi za serikali za mitaa, udiwani, ubunge Tarime Vijijini ...
Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara (CCM) Nyamongo, Kibumaye, Kemakorere, Nyamwaga, Malera na maeneo mengine hawezi kuitisha mkutano kwa vile hakubaliki kabisa amedai kada huyo wa CCM akiongea katika press conference kuhusi hali halisi ya kisiasa Tarime ambapo CCM imedizi kugawanyika na kukosa ushawishi kutokana na kuburuzwa kijeshi hivyo hakuna mikutano, majadiliano wala kukosoana tangu Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara (CCM) aingie ktk siasa za Tarime ...