neno ni upanga
JF-Expert Member
- Jun 28, 2022
- 494
- 1,656
Habari wakuu!
Wiki iliyopita kulikuwa na Waitara Cup ambayo mdhamini wake ni Mwita Waitara. Mshindi wa kwanza alipewa milioni 5 na wa pili nasikia kama milioni 2. Sasa, siku ya fainali mshindi alikuwa ni Sirari au kata ya Sirari. Siku hiyo wakati wanarudi kwao, gari waliyokuwa wamepanda mshindi wa kwanza na mshindi wa pili pamoja na mashabiki wao, yalipata ajali kwa nyakati tofauti.
Cha ajabu, wabeba fedha wote kwenye hayo magari mawili walifariki papo hapo na mbaya zaidi fedha hazikuonekana baada ya hizo ajali mbili na maeneo ni tofauti kabisa. Cha ajabu, sijasikia taarifa ikitangazwa maana majeruhi ni wengi waliojeruhiwa kwenye ajali hii!
Kutokana na hasira hizo, wananchi wamehisi Waitara amefanya kafara, ndo maana amefurushwa huko Sirari. Ikumbukwe Sirari ni ngome ya upinzani ya John Heche.
Source: Nyamwaga Online
=====
Pia Soma:
- Kuelekea 2025 - Tarime: Mbunge Mwita Waitara atimuliwa na Wananchi, ashushwa Jukwaani kwa Fimbo