TUNTEMEKE
JF-Expert Member
- Jun 15, 2009
- 4,587
- 580
Tarehe 28/07/2009 ilikuwa ni siku ya pekee Tarime kwani kulikuwa na maadhimisho ya mwaka mmoja tangu apate ajali na kufariki Mbunge na Mwanaharakati mpigania haki za wanyone Mh. Chacha Zakayo Wangwe "Chacha Rasta".
walichofanya katika siku hiyo ni kuwa na maandamano makubwa hadi katika shule ya Sekondari Nkende, ambayo ni moja ya shule zilizoasisiwa na kujengwa na Kamanda Wangwe akiwa diwani wa kata ya Tarime Mjini mwaka 2004, katika shule hiyo wananchi wa Tarime walipanda miti zaidi ya 30 kama sehemu ya kumbukumbu hiyo.
baada ya hapo waliandamana hadi katika hospitali ya wilaya ya Tarime na kufanya usafi katika mochwari ya kisasa ya wilaya hiyo, kufyeka na kupanda miti pia, kisha wakarudi kwa maandamano na miziki ya reagae na ngoma za asili hadi kwenye uwanja wa mpira wa Tarime kulipokuwa na tamasha la kumuenzi ambapo watu mbalimbali na vikundi vilijitokeza na kutoa burudani kamambe ikiwa na msg za kuthamini kazi aliyoifanya katika uhai wake ya kuwatetea wana Tarime hadi kufungwa huku wakionyesha hisia kuwa kutetea haki kwake ndiyo kumegharimu hata maisha yake.
Tamasha hilo liliandaliwa na Kampuni ya Kind Brothers ikishirikiana na NGO iitwayo Tukamilishane Women Home Association (TUWHA)