KERO TARURA Mbeya hawaoneshi njia mbadala wanapofunga barabara kwa ajili ya ukarabati

KERO TARURA Mbeya hawaoneshi njia mbadala wanapofunga barabara kwa ajili ya ukarabati

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kuna huu mtindo wa Tarura jiji la Mbeya hasa pale wanapofanya marekebisho ya barabara mbovu zile za ndani, huwa wanaweka kibao cha kuonesha barabara imefungwa (kwa watumiaji wa vyombo vya moto) lakini hawaoneshi njia mbadala ya kupita, sasa je wanaomiliki vyombo vya moto watumie barabara zipi?

Pia katika hilo kuna barabara ya mfikemo kutoka barabara kuu ya Tanzania-Zambia kuelekea shule ya msingi Mkapa inafanyiwa ukarabati ni muda mrefu tangu mwaka jana mpaka mwaka huu haijakamilika, wanaotumia vyombo vya moto wanapata usumbufu mkubwa sana.

Kubwa zaidi, sasa hivi wanafanya ukarabati wa hiyo barabara ya Mkapa, lakini wamekuja kuweka kibao cha kuzuia kupita kwenye barabara nyingine eneo la njia panda kuelekea shule ya msingi Maanga karibu na bucha ya Malisa, sasa swali la kujiuliza kwanini waweke kibao cha katazo la kupita kwenye barabara ambayo haifanyiwi ukarabati? Ikitokea mwenye chombo cha moto amepita basi atakamatwa na vijana wa Tarura/jiji wanaotumia pikipiki, na hao vijana wakiwakamata watumiaji wa vyombo vya moto mara nyingi huwaomba RUSHWA ili wasiwapeleke ofisi za Tarura/Jiji.

Wito kwa TAKUKURU kufanya uchunguzi wa tuhuma za RUSHWA kwa wale vijana wanaotumia pikipiki ambao wameajiriwa na TARURA/JIJI LA MBEYA.

Mkurugenzi wa jiji la Mbeya kwa kushirikiana na TARURA wanawajibika kuweka utaratibu sahihi kwa mujibu wa sheria pale wanapofanya ukarabati wa barabara za ndani (lazima waweke njia mbadala na siyo kufunga barabara na kuweka katazo bila kutoa njia mbadala), pia mkurugenzi wa jiji la Mbeya ana wajibu wa kuhakikisha ukarabati huo wa barabara unafanyika kwa muda mfupi na pia anawajibika kuhakikisha barabara zinajengwa katika kiwango chenye ubora kuepusha ukarabati wa mara kwa mara.

imgonline-com-ua-dexifnxJZAjwzTHHV.jpg
 
Njia mbadala mbeya inatokea wapi akati wenyeji walijenga kotekote wakaacha njia za kwenda kuombea moto kwa jilani tu,tarura wanajua wakisema watafute hizo njia miradi haitasonga wakaazi watawahamishia mahakamani.,…acha wafunge
 
Back
Top Bottom