BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Wakala wa Barabara za Vijiji na Mjini (TARURA) Mkoa wa Katavi timizeni wajibu wa kujenga daraja katika Mto Nsemlwa, Manispaa ya Mpanda kivuko kilichojengwa na mtu binafsi kisiwasahaulishe jukumu lenu.
Kivuko kilichojengwa katika barabara inayounganisha Kata ya Nsemlwa, Mtaa wa Migazini na Kata ya Uwanja wa Ndege, Mtaa wa Mnazimmoja hakihimili magari kupita, na ni kikwazo cha Wafanyabiashara kusafirisha bidhaa zao hivyo kudidimiza ukuaji wa uchumi.
Kukosekana kwa daraja ni hatari kwa ustawi wa maisha ya watu hususani pale wagonjwa wasiojiweza kushindwa kusafiri kwa gari kwenda kupata matibabu katika hosptali ya wilaya au mkoa.
TARURA tambueni kivuko kilichojengwa na mtu binafsi kinatoa wito kwenu mtambue umuhimu wa kujenga daraja na mjenge.