TARURA, TANROADS na RC Kunenge kataa uharibifu huu, wana Dar es Salaam tuishi kwa uhuru

TARURA, TANROADS na RC Kunenge kataa uharibifu huu, wana Dar es Salaam tuishi kwa uhuru

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145
Wanna JF,

Tanzania inajipambanua kama kisima cha amani ila watu wake hawana amani. Hii imetokea baada ya kushuhudia kipigo cha mtoza ushuru Wa Magari pale Kariakoo mtaa wa Aggrey, walizozana kwamba machinga anaziba njia kuzuia parking za watu, mtoza ushuru analinda kazi yake maana ukipewa mtaa lazima upeleke pesa vinginevyo huna kibaruamachinga wanawahi asubuhi sana kuziba njia za Magari pamoja na parking, mitaa ya balungombe mtaa wa kongo kote hakupitiki.

Serikali imekuwa ikikosa mapato ya parking kwamba Lila Gari kwa siku ni tshs 2700 Hapo panakaa Magari 20, machinga halipi chichote Bali uzalisha taka zinazoziba mitaro.

Machinga wanaochoma chipsi mafuta humwagwa barabarani, machinga huwa wanawapa kichapo wanaoangusha au kukanyaga vitu kwa bahati mbaya, machinga sasa wamepunguza njia ya mwendo kasi.

Kunenge, TARURA hata kama machinga analindwa kwa sababu tu anapiga kura lakini wapewe basi utaratibu nasi watu huru tuweze kutembea salama kwenye njia halali.

Watu wanavunjwa miguu na pikipiki kwa kuwaendekeza hawa, kwa sasa ukitaka kwenda Kariakoo unajiuliza utafika kweli na kurudi salama.
 
Hao watu ni kero kubwa na ni hatari kwa usalama wa raia wengine.

Unakuta mtu anakaanga chips barabarani na serikali inapita pale na bila kujali madhara yanayoweza kutokea kisa eti wanaongeza idadi ya kura.

Wenye migahawa na mahotel wanasumbuliwa sana na bi au bw afya ktk kuweka mazingira safi ya kwenye majiko kwa kufuata sheria elekezi ya kuwalinda walaji. Je, hawa wanaopika holela kwenye hifadhi za mabarabara hawafuatwi?

Kweli walisema siasa ikiwa mbovu kila kitu kitakuwa kibovu.
 
Wataalam wa afya wanataka biashara zifunikwe, hasa chakula, siku hizi hata Posta unakuta MTU amepanga nyama nje. Kama kwambq jikoni hapatoshi. Alafu wapanga njiani. Ukienda jengo la empress karibu na bismin mwenye hotel kazuia njia halal I kapanga manyama nje. Sijui watu Wa afya wako wapi, mimoshi kila upande.
 
Litafanyiwa kazi haswa kwa kuzingatia misingi ya afya
Pole kwa aliyepigwa
 
Kukaanga chips si bora hivyo gerezani wana pulizia magari rangi kwa compressor barabarani ukipita una vuta hewa yenye rangi!
Kunenga anakazi mzito kupangilia mji uliomshinda makonda, hivi hakuna mkutugenzi anayeweza kumuiga Keenja
 
Acha machinga wapige kazi, Acha ugasho na umbea mtoto wa kiume [emoji16][emoji23]
 
Back
Top Bottom