St. Paka Mweusi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2010
- 7,956
- 5,149
Unaweza kushangaa kwa nini nimepost hapa kwenye jukwaa la siasa.. Lakini huu ni uhujumu uchumi.. Juzi nikiwa Mwenge sokoni mtu wa parking alinielekeza vizuri sehemu ya kupaki gari.
Nikapaki nikafanya ghughuli iliyonipeleka ndani ya dakika ishirini nikawa nimemaliza naondoka.
Jamaa akaja na mashine yake ya kutolea risiti nikampa 500/= akapokea akataka kuondoka, nikamuuliza risiti ipo wapi..?
Nikamwambia naenda sehemu nyingine na ndani ya saa moja ntakuwa nimemaliza shughuli zangu sitaki kudaiwa tena.. Yule jamaa akaniambia mtandao wa Tarula unachukua muda mrefu kutoa risiti.
Nikamwambia ntasubiri. Jamaa akaona isiwe tabu akanirudishia 500/= yangu nikaondoka mpaka Kawe ukwamani.. Kufika Kawe nikamkuta mama mmoja na mashine yake ya kutolea risiti pale Kawe Ukwamani mbele ya duka la nafaka.. Nikapaki vizuri.
Muda mfupi naondoka yule mama anakuja kudai 500/= na risiti hajaweka. Nikamuuliza risiti ipo wapi na yeye akaniuliza kaka na sisi tukale wapi? Nikamjibu bila risiti sikupi hela.
Ndio akatoa risiti akaweka kwenye wipers za gari nikaondoka.. Swali nililojiuliza ni wangapi wenye mchezo huu, na wanawakosesha mapato TARURA kiasi gani kwa siku?
Wenzangu wana JF vipi kwenu, mshakutana na hawa watu wa parking wasio waaminifu..??