Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Baada ya hoja ya Mwanachama wa JamiiForums.com kuhusu kusimama kwa huduma ya Meli ya MV Victoria, ufafanuzi umetolewa, kusoma hoja ya awali bofya hapa ~ Nimekosa huduma ya Meli ya MV. Victoria, inadaiwa haifanyi kazi wiki ya pili sasa, Mamlaka mbona mpo kimya?
MAELEZO YA KAMPUNI YA MELI
JamiiForums imewasiliana na Anslem Namala ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) amesema:
Kilichofanyika ni kusimamishwa kwa huduma kwa ajili ya matengenezo ya kawaida ambayo yanafanyika mara moja kwa mwaka, mara nyingi hali hii inafanyika wakati wa kipindi kisichokuwa na wasafiri wengi kama ilivyo sasa.
Huduma mpaka sasa zimesimama kwa tarkibani wiki moja, kilichofanyika ni kuangalia na kufanya ukaguzi wa juu, kuanzia kesho tutaipandisha juu kwenye chelezo kwa ajili ya kuanza ukaguzi wa chini.
Hivyo, Watu wasiwe na wasi ni ukaguzi wa kawaida kama inavyofanyiwa gari inapomaliza zile kilometa zake.