Task force ya kupambana na ujangili nchini kuendeshwa kwa miemko ya kisiasa.

Task force ya kupambana na ujangili nchini kuendeshwa kwa miemko ya kisiasa.

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe kupambana na tatizo la ujangili, kimetuhumiwa kutumika na baadhi ya wanasiasa na watumishi mbalimbali wa serikali ili kutekeleleza malengo mbalimbali ya kisiasa.

Kikosi hicho ambacho wiki iliyopita Rais Magufuli alikipongeza kwa kazi nzuri na kukitaka kijikite katika kuhakikisha watuhumiwa wote wanakamatwa bila kujali nyadhfa zao, kimetajwa kutumiwa na aliyekuwa Mbunge wa Mbarali na mgombea ubunge kwa tiketi ya ACT-Wazalendo uchaguzi uliopita, bwana Dickson Kilufi, dhidi ya mpinzani wake, mbunge wa sasa, Haroon Mulla wa CCM.

Mpango huo ambao unatajwa kusukwa na aliyekuwa meneja wa kampeni wa Kilufi, Dk. Anthony Mwandulami, ukiwa na lengo la kumchafua mpinzani wao,Ndugu Mulla, ambaye pia wamemfungulia kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi ya jimbo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Dk.Mwandulami ambaye pia ni mfanyabiashara na mganga wa kienyeji, amekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na Mkuu wa Kikosi cha Kupambana na ujangili, bwana Robert Mande na inaelezwa ni kumpa taarifa za upotoshaji kuhusu uhusika wa mbunge huyo katika ujangili.

Upotoshaji wa taarifa aliopewa waziri Maghembe pamoja na bwana Mande, ulipelekea kikosi maalumu kupekua nyumba na shamba la mbunge huyo ambapo hata hivyo hakuna ushahidi uliopatikana.

‘Kuna jambo lipo nyuma ya swala hili zima, hasa ukizingatia uhusika wa Dk.Mwandulami, mlolongo wa matukio, pamoja na uwepo wa taarifa nyingi zinazochanganya’ alisema mtoa taarifa huyo.

Taarifa nyingine zilizoripotiwa na baadhi ya magazeti wiki hii pia zimezidi kuleta mkanganyiko na pamoja na hali ya sintofahamu hasa kutokana na majina kadha wa kadha yanayotwajwa kama Mpemba na Mangi kuwa yanahusika na matukio ya ujangili.

Wahusika hao ambao bado hawajajulikana wasifu wao, ili kutovuruga uchunguzi, kwa mujibu wa Waziri, kumechochea kuongezeka kwa upotoshaji mkubwa miongoni wanajamii.

Mtoa taarifa huyo ameenda mbele zaidi kwa kuiomba serikali na waziri kuwa makini na upotoshaji wa taarifa na pia kutokuhusisha maslahi ya kisiasa katika kupambana na matukio ya ujangili, ambayo yemeitikisa nchi yetu kwa kipindi kirefu.
 
Back
Top Bottom