Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,286
{Mmoja wetu punguani, ana matobo kichwani
Alipofika duniani, mbingu purukushani
Tangu hapo tafrani, amani hapatikani,
Amani si amani, anadanganya punguani
Filosofa wa Kundavi, Dotto na wengine,
Semeni pasi chumvi, mnipoze nami none,
Wamjue wetu mwivi, alopea kwa unene
Nipeni mji kishindwa, huyu nani punguani?}
Hilo juu ni shairi alilotunga Kamanda Bonomali Luziga. Kazi za huyu Bwana nazikubali sana, kwani zinaandaliwa kwa upeo mkubwa ingawa yawezekana yeye mwenyewe akadhani ni upeo wa kawaida. Pamoja na mambo mengine ambayo yanaonekana katika maudhui ya shairi hilo, shairi hilo linamtaja punguani na mambo aliyoleta huyo punguani mbinguni na duniani, vyovyote iwavyo, huyu punguani anayetajwa katika shahiri hili atakuwa ni Ibilisi.
Kwakuwa katika ubeti wa pili mshahiri amenitaja kwa jina huku akisisitiza kuwa nimtaje huyo punguani ni nani ambaye yuko na matobo kichwani, hivyo basi kwa heshima na taadhima aliyonipa kamanda Luziga, naomba nimtaje huyo punguani huku nikiacha swali kwa lengo la kutanua mjadala. Naomba soma shairi langu hapo chini lenye jibu na swali langu kwenu.
MUNGU NI PUNGUANI NA BABA WA HUO?
Nimezama fikirani,
Kumsaka Punguani,
Alozua tafrani,
Mbinguni na duniani,
Nimemjua jamani,
Huyo Bwana Punguani.
Ameuumba nani?
Huu upunguani,
Nacho kiumbe jamani,
Kilichopo duniani,
Kina milanga jamani,
Naam tangu zamani.
Ukisoma Qur-ani,
Biblia kwa makini,
Kila kitu duniani,
Kimeumbwa na Manani,
Hivi upunguani,
Ameuumba nani?
Huwezi umba tufani,
Na usiwe majinuni,
Muumba upunguani,
Tuumpe cheo gani?
Kama si yeye jamani,
Tungeujua upunguani?
Nimezama methalini,
Kwa mfalme Sulemani,
Mungu kafanya shetani,
Kwa siku ya ushetani,
Je, haya mapunguani,
Kwa siku ya upunguani?
Kila kitu duniani,
Ni upuuzi jamani,
Kula upepo kinywani,
Hata yale ya makini,
Yote sawa jamani.
Yana faida gani?
Kuna moja la zamani,
Lamfika punguani,
Mwenye akili makini,
Na mwenye jeshi makini,
Kifo huwapiga chini,
Akili za wafaani?
Hilo moja la zamani,
Katu halimfiki Manani,
Jambo hili wenzanguni,
Katu halifuti yakini,
Kuwa kaumba Manani,
Huu upunguani.
Kamtia upunguani,
Ibilisi rasini,
Akawa hayawani,
Mtia ulimi puani,
Akazua tafrani,
Mbinguni na duniani.
Kilichopo rasini,
Mwa Ibilisi jamani,
Amekiumba nani?
Tafauti na Rahmani,
Ndicho chanzo jamani,
Cha huu upunguani.
Mungu ni punguani?
Na baba wa huo jamani?
Nipeni jibu makini,
Ni wapi ukafirini?
Huo mji wa motoni,
Sitaki fika asilani.
Luziga toka fichoni,
Nikutie machoni,
Ule mji wa zaituni,
Nautaka si utani,
Nipate kula tini,
Ukikosa jibu makini.
Na wengine karibuni,
Katika huu mtihani,
Malenga wapya njooni,
Na wale wazamani,
Mungu ana cheo gani?
Kama si punguani?
Wino wa zafarani,
Umeisha chupani,
Ya manjano zafarani,
Iliyokwisha si utani,
Loo!!! niko mwishoni,
Poo! ni tamatini.
Njano5
0715845394.
Alipofika duniani, mbingu purukushani
Tangu hapo tafrani, amani hapatikani,
Amani si amani, anadanganya punguani
Filosofa wa Kundavi, Dotto na wengine,
Semeni pasi chumvi, mnipoze nami none,
Wamjue wetu mwivi, alopea kwa unene
Nipeni mji kishindwa, huyu nani punguani?}
Hilo juu ni shairi alilotunga Kamanda Bonomali Luziga. Kazi za huyu Bwana nazikubali sana, kwani zinaandaliwa kwa upeo mkubwa ingawa yawezekana yeye mwenyewe akadhani ni upeo wa kawaida. Pamoja na mambo mengine ambayo yanaonekana katika maudhui ya shairi hilo, shairi hilo linamtaja punguani na mambo aliyoleta huyo punguani mbinguni na duniani, vyovyote iwavyo, huyu punguani anayetajwa katika shahiri hili atakuwa ni Ibilisi.
Kwakuwa katika ubeti wa pili mshahiri amenitaja kwa jina huku akisisitiza kuwa nimtaje huyo punguani ni nani ambaye yuko na matobo kichwani, hivyo basi kwa heshima na taadhima aliyonipa kamanda Luziga, naomba nimtaje huyo punguani huku nikiacha swali kwa lengo la kutanua mjadala. Naomba soma shairi langu hapo chini lenye jibu na swali langu kwenu.
MUNGU NI PUNGUANI NA BABA WA HUO?
Nimezama fikirani,
Kumsaka Punguani,
Alozua tafrani,
Mbinguni na duniani,
Nimemjua jamani,
Huyo Bwana Punguani.
Ameuumba nani?
Huu upunguani,
Nacho kiumbe jamani,
Kilichopo duniani,
Kina milanga jamani,
Naam tangu zamani.
Ukisoma Qur-ani,
Biblia kwa makini,
Kila kitu duniani,
Kimeumbwa na Manani,
Hivi upunguani,
Ameuumba nani?
Huwezi umba tufani,
Na usiwe majinuni,
Muumba upunguani,
Tuumpe cheo gani?
Kama si yeye jamani,
Tungeujua upunguani?
Nimezama methalini,
Kwa mfalme Sulemani,
Mungu kafanya shetani,
Kwa siku ya ushetani,
Je, haya mapunguani,
Kwa siku ya upunguani?
Kila kitu duniani,
Ni upuuzi jamani,
Kula upepo kinywani,
Hata yale ya makini,
Yote sawa jamani.
Yana faida gani?
Kuna moja la zamani,
Lamfika punguani,
Mwenye akili makini,
Na mwenye jeshi makini,
Kifo huwapiga chini,
Akili za wafaani?
Hilo moja la zamani,
Katu halimfiki Manani,
Jambo hili wenzanguni,
Katu halifuti yakini,
Kuwa kaumba Manani,
Huu upunguani.
Kamtia upunguani,
Ibilisi rasini,
Akawa hayawani,
Mtia ulimi puani,
Akazua tafrani,
Mbinguni na duniani.
Kilichopo rasini,
Mwa Ibilisi jamani,
Amekiumba nani?
Tafauti na Rahmani,
Ndicho chanzo jamani,
Cha huu upunguani.
Mungu ni punguani?
Na baba wa huo jamani?
Nipeni jibu makini,
Ni wapi ukafirini?
Huo mji wa motoni,
Sitaki fika asilani.
Luziga toka fichoni,
Nikutie machoni,
Ule mji wa zaituni,
Nautaka si utani,
Nipate kula tini,
Ukikosa jibu makini.
Na wengine karibuni,
Katika huu mtihani,
Malenga wapya njooni,
Na wale wazamani,
Mungu ana cheo gani?
Kama si punguani?
Wino wa zafarani,
Umeisha chupani,
Ya manjano zafarani,
Iliyokwisha si utani,
Loo!!! niko mwishoni,
Poo! ni tamatini.
Njano5
0715845394.