Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,286
Ugaidi ni nini hasa? Kuna uhusiano gani kati ya uislamu na ugaidi? Kuna uhusiano gani kati ya Marekani na ugaidi? Hivi Somali kuna shida gani? Hivi ilikuwaje Kenya ikajitia kwenye mgogoro na Somali? Mwenye kujua hayo na anijuze.
Nasikitika kuona dunia ikipambana na ugaidi badala ya kung'oa mizizi ya ugaidi. Huwezi kuzungumzia ugaidi kisha usizungumzie nchi za Afghanstan, Somali, Iraq, Pakistan, Palestina, Israeli, Saud Arabia, na Marekani.
Ukichunguza kwa makini ugaidi ni matokeo ya kuangushwa kwa tawala za nchi au majimbo zisizofuta siasa za kimagharibi(Demokrasia) au zilizokaidi kuwa vibaraka wa umagharibi. Tawala hizi ziliangushwa na badala yake zikasimikwa tawala zinazofuata mfumo wa demokrasia au zile zilizofyata mkia kwenye mikono ya wamagharibi.
Katika vita hakuna mshindi wala mshindwa, bali kuna kurudi nyuma na kujipanga. Kwenye mazungumzo ndio yupo mshindi; mshindi ni yule aliyefanikiwa kujenga hoja zenye mashiko hata mshindani wake akazielewa na kuacha hoja zake mufilisi. Katika mazungumzo mwenye kukubali kushindwa hubaki kwa furaha kwani anajua amekubali jambo lenye kumfaa.
Watu wamagharibi wanadhani kuwa mfumo wa kidemokrasia ndio mwarobaini wa shida zote za mwanadamu, na pia wanadhani kila sehemu yenye rasilimali wanaweza kuingia watakavyo hata ikibidi kwa mabavu. Mienendo ya nchi za kimagharibi ndio chanzo cha machafuko makubwa yote yaliyowahi na yanayoendelea kutokea ulimwengu.
Tukiwa kama dunia hatujasaahu biashara utumwa iliyoitajirisha Ulaya, lakini hadi sasa lawama kwa biashara ile kwa hapa Afrika Mashariki kaibeba mwarabu kama vile mashamba ya buni kule bara Amerika yalikuwa mali yake, ukoloni, vita ya kwanza ya dunia na ya pili. Hayo yote yaliinufaisha Ulaya na si mashariki au Afrika yenyewe. Katika ulimwengu wa ukoloni mamboleo zile nchi ambazo hazitaki kuwa vibaraka wa magharibi basi zitaundiwa kila aina ya zengwe ikiwemo na zengwe la kuzisema hizo nchi hazifuati utawala wa kidemokrasia au zina silaha za maangamizi.
Libya ya Ghadafi, ilikuwa ni nchi inayoongozwa vizuri pamoja na kwamba kulikuwa hakuna utawala wa kidemokrasia. Wananchi wa Libya walikuwa wanaishi vizuri na kuthaminiwa na serikali yao kuliko hata sisi watanzania tuliokuwa na serikali ya kidemokrasia. Tatizo la Ghadafi ni kukataa kwake kuwa kibaraka wa nchi za magharibi na yale maandamano na uasi umedhaminiwa na wamagharibi. Ukorofi wa Ghadafi ni kuona rasilimali za Libya zinawafaa zaidi walibya kuliko wazungu, Sasa hivi walibya wanajuta, wanatamani Ghadafi harudi hata sasa.
Hebu niambie, kwa wale wafuasi wa GHADAFI wakianza kulipiza kisasi dhidi ya serikali ya Tripoli ya sasa, Marekani na nchi za magharibi ni kosa? Ndio maana sikushangaa na wala sikusikitika pale ubalozi wa Marekani katika nchi ya Libya uliposhambuliwa. Iweje upande upepo kisha ughairi kuvuna tufani? Hichi ndicho kilichotokea Somali, Afghanstan na Iraq na sehemu zingine nyingi ambazo ziko na machafuko. Kung'olewa kwa tawala zile kimabavu huku Marekani ikishiriki aidha kwa chinichini au dhahiri ndio chanzo cha hii sinema ya ugaidi na vita dhidi ya ugaidi inayoendelea duniani.
Badala ya dunia kuamua kupambana na huo ugaidi kwa kudhamiria kuyapoteza makundi na magenge ya kigaidi kama Al-shababi na Al-qaida, ni vema dunia kwa nia ya dhati ikawakutanisha makundi yanayokinzana dhidi serikali, katika nchi za Afghanstan, Somalia na Iraqi, na wakati huo huo mgogoro kati ya Palestina na Israeli, na matatizo yaliyo katika nchi ya Chechinyia yapatiwe ufumbuzi. Matatizo na migogoro katika sehemu nilizozitaja hayawezi kuisha kwa nguvu za kijeshi ambazo Marekani inajivunia nayo.
Sehemu hizo zote ukizichunguza kwa makini utagundua kuwa tawala zake zilikuwa zinafuata sharia au zilikuwa hazikubali kuwa vibaraka wa magharibi. Wamarekani hawataki kusikia na wala hawapendi kuziona tawala zinazofuata sharia ya kiislamu na pia hawapendi tawala ambazo hazikubali kuendeshwa na wamagharibi. Kwa msingi huu, tatizo si ugaidi tatizo ni aina mpya ukoloni unaosambazwa na wamagharibi, kwani, kwa vyovyote vile ukoloni huu ndio chanzo cha ugaidi. Haya makundi yanayoitwa ya kigaidi huenda yanapambana na huo ukuloni mpya.
Serikali za Afrika ni za kinafiki sana na wapo kama mizombi kwa kukubali kuendeshwa. Kwa akili zao wanafikiri tatizo la Somalia linaweza kumalizwa kwa kutumia nguvu za kijeshi. Ukiangalia maumbile ya tatizo kati ya CONGO DRC na Somalia ni rahisi sana kulimaliza kijeshi tatizo DRC kuliko Somalia. Mabavu yaliyotumika dhidi ya Alshababi na wasomalia kwa ujumla kabla hata ya vikosi vya Afrika kuingia Somalia vinaumiza sana.
Video zinazoonesha yalitokea wiki hii Kenya zinatia machozi, lakini pia video zinazoonesha wasomalia wanavyofanyiwa vibaraka wa magharibi na wakati mwingine na majeshi ya kigeni pia zinaumiza na kuliza sana. Wasomali wakati mwingine hata kufanya ibada kwao ni tabu. Wakati nchi za Afrika zinapeleka vikosi Somali pia zingefikiria namna ya kuumaliza mgogoro wa Somalia kimazungumzo na si kutumia ubabe kama inavyofikiri Marekani.
Nimechukizwa na vitendo walivyovifanya Al-shabi Kenya, wangeipiga na kuvamia Ikulu ya Kenya nisingeumia hata kidogo, lakini kitendo cha kuua watu wasio na hatia binafsi kwa sasa nashindwa kuitafautisha hiyo Al-shababi na Marekani. Huenda hasira za Al-shababi kwa serikali ya Kenya zikawa ni za haki, lakini wale watu waliokufa na kujeruhiwa kwa tukio lile ndio watunga sera au ndio serikali ya Kenya? Huu ni uonezi dhidi ya utu wa mtu uliodhahiri na katu si wa kuungwa mkono. Marekani imeua maelfu ya watu wasio na hatia huko Iraq na Afghanstan nayo Al-shababi yafanya unyama uleule kama wa Marekani.

Watu hawa hata ugomvi kati ya Al-shababi na Serikali yao hawajui na hauwahusu, lakini wameuliwa kinyama na kuumizwa kinyama, Mungu awalaani wote wanaofanya unyama huu,,pamoja na hayo, nani katudanganya kuwa vita ina macho?
Na ilaaniwe ile siku niliyozaliwa.
Njano5
0784845394.