Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,286
Ashiki majinuni, Fatma bint Subiani,
Nampenda moyoni, sisikii wala sioni,
Ameketi kitangani, na chano chake pembeni,
Naanza alif, bee, tee, jamani natia kikomo.
Kitezo, uvumba, ubani, na udi wa Marohani,
Halititi, mashtaka, zafarani, na kisinda jini,
Shime viwepo chanoni, ni muhimu jamani,

Maji ya zamda chupani, sanamaki ya kusini,
Kamla swedi, giligilani, na vizimba vya pwani,
Manemane jamani, na mkongojo jini,

Ya Rabi Mola Sultani, cha mtu sitamani,
Hata niwe shakani, ngome yangu Rahmani,
Ameumba mashetani, kwa siku ya ushetani?

Niwe na mbawa tisini, nipae hata mbinguni,
Hata kwa kufika arshini, qadar sitaipiga chini,
Hata kwa dua makini, qadar hawezekani?

Fatma mwana wa jini, ni yangu qadar jamani?
Kwani niko shubuani, na hii mingi mitihani,
Habanduki ubavuni, wala hatoki rasini.

Nimezama misahafuni, na sherehe za wanazuoni,
Biblia na Qur-ani, na maandishi ya zamani,
Naitafuta yakini, iliyothibiti vitabuni.

Fatma wewe ni nani, na hasa wataka nini?
Vilaji vi chanoni, sema sasa ya moyoni,
Au nizame nyotani, nijue ya ghaibuni?

"Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya." mithali 16:4
Kama kawa nipo juu ya farasi wa mnjano nikielekea safari ya mbali nisiyoijua mwanzowe wala mwishowe, mimi na njia, njia na mimi, naam kama lila na fila. Nijuacho ni kimoja, ya kwamba natakiwa kufika katika ufalme wa Manjano, huko natakiwa kwenda kumfunda bint mfalme kabla hajatiwa mafuta kuwa Malkia wa himaya ya Manjano. Kuna vihunzi na vikwazo vingi, vyovyote iwavyo, yaani hata kwa saini ya kifo, lazima nifike huko, kwani mtukufu Mfalme na Binti Mfalme wananisubiri kwa shauku kubwa, niko na imani inshallah nitafika.
Niko pekupeku, nimevaa kanzu nyepesi ya njano na suruali ya njano, sehemu chache za kifua changu ziwazi, hii ni kutokana na upepo unoisuka kanzu yangu isiyokuwa na vishikizo, vinywele vya kipilipili vilivyoota kifuani navyo havisalimika na jazuo la upepo huu. Mwendo wa farasi hausemi urongo, tatizo safari haina kikomo, kinyume chake ningekuwa nishafika niendapo kitambo.
UTENZI HUU UNAHADITHIA JAMBO LA KWELI LINALONIHUSU MWENYEWE, LENGO NI KUTUNGA BETI 3500. NITATUNGA KIDOGO KIDOGO KISHA NITAKUJA KUZIUNGANISHA.
ITAENDELEA......
Njano5
0715845394/0762845394/0784845394