Nimefanikiwa kuhudhuria kwa miaka mitatu mfululizo maonesho ya nane nane Morogoro,kwa kweli napenda kusema wahusika hawavitendei haki viwanja hivi,hawawatendei haki waudhuriaji na hata hawawatendei haki wenye mabanda na taifa kwa ujumla,achilia mbali kutoyapa hadhi mashindano yenyewe!viwanja hv miaka nenda miaka rudi vimekua ni vichafu,na vumbi lililopitiliza kiasi cha kufanya wale wepesi wa kupata matatizo ya mafua na kifua,kukumbana na kadhia hiyo mara watokapo kwenye viwanja hivyo!cha kusikitisha,wahusika wamekua wakipata hela nyingi mno kutoka kwa waudhuriaji,na hata wale wakodishao mabanda,lakini haieleweki hela hizo zinakwenda wapi kiasi cha kushinda hata kufanya maboresho kidogo japo kwa awamu,ikiwemo kumwaga hata changarawe kwenye njia,kuboresha vyoo angalau wananchi nasi tuamini kua mapato hayo yanatendewa haki,na maonesho hayo yanathaminiwa!pia nimesikia ndani ya viwanja hivyo vya maonesho kuna viwanja vinauzwa kwa watu binafsi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba binafsi,ili limeshindwa kuniingia akilini kua lina dhamira gani hasa!