Taso boresheni nane nane Morogoro

Farmer82

Senior Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
183
Reaction score
39
Nimefanikiwa kuhudhuria kwa miaka mitatu mfululizo maonesho ya nane nane Morogoro,kwa kweli napenda kusema wahusika hawavitendei haki viwanja hivi,hawawatendei haki waudhuriaji na hata hawawatendei haki wenye mabanda na taifa kwa ujumla,achilia mbali kutoyapa hadhi mashindano yenyewe!viwanja hv miaka nenda miaka rudi vimekua ni vichafu,na vumbi lililopitiliza kiasi cha kufanya wale wepesi wa kupata matatizo ya mafua na kifua,kukumbana na kadhia hiyo mara watokapo kwenye viwanja hivyo!cha kusikitisha,wahusika wamekua wakipata hela nyingi mno kutoka kwa waudhuriaji,na hata wale wakodishao mabanda,lakini haieleweki hela hizo zinakwenda wapi kiasi cha kushinda hata kufanya maboresho kidogo japo kwa awamu,ikiwemo kumwaga hata changarawe kwenye njia,kuboresha vyoo angalau wananchi nasi tuamini kua mapato hayo yanatendewa haki,na maonesho hayo yanathaminiwa!pia nimesikia ndani ya viwanja hivyo vya maonesho kuna viwanja vinauzwa kwa watu binafsi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba binafsi,ili limeshindwa kuniingia akilini kua lina dhamira gani hasa!
 
Yaani miaka kibao hakuna uboreshwaji. Kuhusu viwanja nimesikia tena nilivifukuzia nikachelewa viwanja lak 3 tu
 
Yaani miaka kibao hakuna uboreshwaji. Kuhusu viwanja nimesikia tena nilivifukuzia nikachelewa viwanja lak 3 tu

Kwa hiyo wanapouza hivyo viwanja ndani ya uwanja wa maonesho nini hatima ya maonesho hayo?kwa kweli viwanja vile vya nane nane Morogo ni aibu kubwa,wahusika hizo hela lukuki wanazopata sijui wanazitupa wapi,hata maboresho ya kuzuga tu yangetosha,bad enough yamekua ni kama gulio la wamachinga kwenda kumwaga bidhaa zao! Ili taifa bado lina mwendo mrefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…