wanafunzi wa TATAKI inaonekana wamekurupuka bila kufuata hatua stahiki. Nilishangaa yule dada mfupi mweusi kiaina alivyokua anapiga kelele na kuahamsisha wenzie wapige kelele lakini baadae ndiyo wa kwanza kuyeyuka. Tuongee ukweli hapa na tujadili uhalisia wanajamii, hivi vita yote hiyo ni ya kutaka uwadani (Practicle training) au kutaka pesa za uwadani? Kimsingi tuko kipesa zaidi na siyo kielimu. Tutambue kuwa package ya course mpaka ipitishwe na seneti lazima iwe inakidhi mahitaji ya mwanafunzi na ndiyo maana wenzetu wa sheria wanaenda field baada ya kumaliza chuo (law school). Uhauri wangu ni kuwa wanatataki tusihangaike sana kubishana na wenye makali kwa staili ya kutumia nguvu maana mwishoni wataona nia yenu ni pesa na siyo elimu hivyo wanaweza kupeleka pendekezo kuwa asiyeweza kusoma hii kozi bila kwenda uwadani aache chuo au kuifuta moja kwa moja. Tukumbuke na tujiulize UDOM ilikuaje na sasa wako wapi? Yatupasa kutumia akili na maarifa zaidi. Viongozi waandike mswada (concept) utakaoanisha dhumuni halisi na umuhimu wa uwadani wakianzia na mawazo wa nafunzi wote, walimu wao ndio iende ngazi kwa ngazi hadi ifike kwa mwenyekiti wa seneti la sivyo tutaandikia mate wakati wino tunao.