Zanzibar 2020 Tathmini fupi mara Baada ya uteuzi wa Dkt Hussein Mwinyi huko NEC ya CCM

Bado napata kigagaziko kwa ccm kuendelea kutoa urais kwa watoto wa maraie. Huu ni upuuzi Sana. Mwinyi Hana kitu unique zaidi ya kuwa babake alikuwa Rais. Si ajabu baba alikuwa anaunga mkono juhudi daily hata Mambo ya ajabu.
Kwa ccm maana yake wote hawana akili isipokuwa watoto wa marais wastaafu.
 
Mimi iki kitu ndio huwa sielewi mgombea wa uraisi zanzibar anapitishwa na nec bara ..kwa nini nec zanzibar wasikae wakapitisha mtu wao huko ndio aje bara wasalimu
Hakuna NEC bara wala NEC Zanzibar, kuna NEC moja tu CCM. Kasome katiba ya CCM uongeze ufahamu.
 
Hii tabia ya Tanganyika kuwaamulia wazanzibari hadi rais wao inaniudhi sn.....

Kwa nini lkn?
Na itaendelea kukuudhi kila leo kwasabb ndiyo utaratibu wa chama
 
Tathimini nzuri lakini haikamiliki mpaka utupe ya seifu sharif nae ni chaguo la wapi?!
 
Acheni nongwa
Wagombea walikua 31,wamechujwa na kubaki watano
Wagombea ni wazanzibari,wachujaji ni wazanzibari
Dodoma.yameletwa majina ya wazanzibari watano,ni lazima apite mmoja
Acheni nongwa
Yamechujwa vipi? Walipigia kura wapi hayo majina matano? Kila mtu anajua hayo majina yamepatikana kwa SHINIKIZO kutoka bara. Zanzibar ndio inakufa hivyo, Wazanzibari chukueni hatua haraka.
 
Binafsi sijaona chochote cha ziada alichonacho Dr Hussein Mwinyi, amekaa wizara ya ulinzi kwa muda mrefu lakini hakuna cha maana alichofanya, kashindwa hata kuwasaidia watu wake ambao wanamatatizo lukuki. Kilicjombeba na histori ya kuwa mtoto wa rais mstaafu
 
Wazanzibar waache kwanza kubaguana wao kwa wao ili kulinda maslahi yao la sivyo wataendeshwa tuu
 
Mkuu hapo ulipoandika (kwaheri zanzibar !usiniulize kwanini) umenitafakarisha halafu sijaelewa kabisa!!
hii mbona iko wazi tu suala la kudai mamlaka kamili au angalau kuongezwa nguvu ya Zenji mchakato utaanza tena after ten years baada ya Mwinyi Junior ni mgeni kabisa kwao na ambae ni mzanzibara!!
yaani yoyote atakaehoji kuhusu mamlaka kamili ya Zenji na kuvunja muungano atavunjwavunjwa yeye na FFU na JWTZ!!
 
So, una maanisha m'kiti alikuwa sahihi kumpendekeza mnyaa zidi ya mwinyi? nieleweshe mkuu.
 
Wananzibari wanachaguliwa raisi wao kutoka Tanganyika, how ironic!!!
Mtasema sanaaa na wala hatamshinda. Hao wagombea watano kwani wamechaguliwa wapi..Jomba sikuelewi.which means all five candidates had equal chances of being selected.chama ni kimoja kina cut across bara na zenj. Na mshindi lazima awe mmoja tu. Sasa unataka kutuambia nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ