Zanzibar 2020 Tathmini fupi mara Baada ya uteuzi wa Dkt Hussein Mwinyi huko NEC ya CCM

Niliongea hili kuwa Prof na mkulu zinapanda sana ila Sio kwa extent hio ya Kumtema JR ambapo wote ni mashahidi SR anavyolamba Viatu, Hawa wastaafu ni muhumi sana haswa kipindi hichi
Japo Mkulu angeamua kuzinda akapiga chini JR na kwenda Prof bado wasingemtisha japo ingetokea collision ila hao ni wastaafu tu effect yao ni negligible japo inshu ya fadhila ni muhimu kwa vile na wewe una watoto pia
 
Sasa ajabu utasikia hizo Unguja A, B na C kila moja ina watu elfu tano. Hao ukiwaachia nchi si watazikana usiku mmoja tu.

Mimi nilijua Kuna Unguja na Pemba tu.

Kumbe kuna Unguja kusini,Unguja Kaskazini,Unguja Magharibi na Unguja kati.

Mmewabagua wapemba hadi mmeanza kujibagua wenyewe...

Kweli dhambi ya ubaguzi haijawahi kuacha wabaguzi salama.
 
Mada kama hizi huwa zinanipa shida sana.

Hubidi nibadili mawani mara tatu ili nisome na kuzielewa, lakini wapi, nabaki na kichwa kinazunguka tu mwisho wa kuzisoma.
Plan A ilikuwa Prof, Plan B ni Dkt Mwinyi ili kulinda maslahi ya Bara.

Hiyo plan B ilikuja baada ya upepo kubadilika. Namba ilikuwa hazisomi
 
Wao ardhi yao ukitoka bara ukienda nunua kule awataki ila wao uku bara wana maeneo kibao ok any way uwo ni ubinafsi kama wanataka na wao waje wagombe Tanzania bara.
 
Kweli hao watu laana ya ubaguzi inawatafuna Haswaa!
Wakoloni wote walitengeneza Sera ya divide and rule. Hata wakoloni weusi ndio usiseme.

Ndio maana juhudi za Akina Rais Karume JR na Maalim Seif za kuunda GNU hazikuwafurahisha agents was mkoloni mweusi.
Hao akina Jecha na kisa cha uchaguzi wa marudio ni mifano tu.

Hata waliowalinda kwa magari ya deraya na vifaru na kuongoza serikali kinyume cha katiba utawajua kuwa wanaendeleza device and rule.

Wazanzibari wamebebeshwa utumwa wa historia.

Maskini hata vizazi visivyohusika wanabeba mzigo huo
 
NEC ya CCM imepitisha Rais wa Znz, kazi ya Mkutano mkuu leo na Wa znz hapo October ni kubariki tu uamuzi
 
Habari, jukwaa hili lazima liongozwe kwa weledi, hesabu hazidanganyi! Weka idadi ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa na mchanganuo kwa watokao i.e. Bara ua Zanzibar ili twende sawa. Je Zanzibar ina asilimia 20% tu ya wajumbe wote wa NEC hapana.
 
Mimi iki kitu ndio huwa sielewi mgombea wa uraisi zanzibar anapitishwa na nec bara ..kwa nini nec zanzibar wasikae wakapitisha mtu wao huko ndio aje bara wasalimu
CCM ni Moja ,ina Ofisi ya Makao Makuu Dodoma , na Ofisi mbili za makao Makuu 1.Lumumba Dsm na 2.Kisiwandui Unguja. Vikao vya Chama pia havigawanyiki ila kuna Kamati maalum ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC), lakini NEK kama kikao cha maamuzi ni kimoja, na maamuzi yake ni hayanauhusiano na eneo kikao kinapofanyika iwe Zanzibar, Dodoma,Mwanza ,DSM nk.
 
Kwa taarifa tu tangu mwanzo CCM iliweka uwiano wa idadi ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa. A).Wajumbe kutoka mikoa A.1) Zanzibar mikoa 5 ,wajumbe wanne kila mkoa = 4 X 5 =20, A.2) Tanzania Bara , mjumbe mmoja kila mkoa = 1 X 20 =20. Hali ilikuwa hivi tangu wakati wa mwalimu. Kwa sasa idadi ya mikoa Zanzibar iko hivyo hivyo yaani mitano na wajumbe ni 20, upande wa Tanzania Bara mikoa imeongeza na kuwa 26 ,hivyo waNEK watakuwa 26.
B) Viongozi wakuu wa Chama B.1) Wenyeviti wa Chama yaani Mwenyekiti na Makamu wake = 3, uwiano ni 1:2 kutegemea mwenyekiti anatoka sehemu gani ya Muungano, B.2) Makatibu wa Chama yaani Katibu na Manaibu Katibu Mkuu wake = 3, uwiano ni 1:2 kutegemea katibu Mkuu anatoka sehemu gani ya Muungano,
C.) Wajumbe nafasi Ishirini (20) za Taifa (kapu), C.1)kumi (10) bara , na C.2) kumi (10) Visiwani,
D) Wajumbe Kutoka Jumuiya za ChamaD.1) Vijana , D.2) Wanawake ,D.3 Wazazi ,zotezipo kw auwiano.
Kwa ujumla siyo sahihi Bara kuiamulia Zanzibar.
 
Sasa ajabu utasikia hizo Unguja A, B na C kila moja ina watu elfu tano. Hao ukiwaachia nchi si watazikana usiku mmoja tu.
Zanzibar ina watu zaidi ya Million moja, makadirio yako ya buku tano tano ni batili.
 
Wanaosema hivyo ni wapinzani. Asilimia 80 ya kura ni wazanzibar
 
Issue sio kugombea huku bali kuwaamulia rais wa Zanzibar sio sawa kabisaa
Nchi ni moja, Chama ni kimoja, Halmashauri kuu ya Taifa ni moja, kama Bunge lilivyo moja! huwezi kusema leo tunajadili issue ya Zanzibar wengine wote msiotoka Zanzibar tokeni mtupishe! Naomba uzoefu wa vyama vingine kama Chadema, CUF ,NCCR , ADC ,Jahazi Asili vyote hivyo vilifasimamisha wagombe urais Zanzibar , je ukifika wakati wa maamuzi huwa wanafakuza wajumbe wa vikao vya maamuzi wabaki wa Zanzibar tu?!
 
siasa duniani kote ni hadaa tu uhalisia katika siasa labda upo mbinguni,Hakuna cha mfumo wala Baba jesaca,Mkapa na Kiwkete wamisha kaa wakakubaliana kuwa rais awe mwinyi na ndivyo alivyokuwa hata bara 2025 ndivyo itakavyokuwa hadi siku wakifa.
 
Hii tabia ya Tanganyika kuwaamulia wazanzibari hadi rais wao inaniudhi sn.....

Kwa nini lkn?
Si kweli. Majina yote yamependekezwa na Kamati Maalum ya NEC. Hao ni Wazanzibari watupu. Majina hayakubuniwa Dodoma! Hata hivyo hakuna chama makini cha siasa ulimwenguni kinachoachia sehemu ya nchi imteue mwakilishi wake muhimu bila kuhusisha ngazi ya taifa. Inatokea sasa hivi chaguzi za Amerika kwa maseneta wa majimbo (states).
 
siasa duniani kote ni hadaa tu uhalisia katika siasa labda upo mbinguni,Hakuna cha mfumo wala Baba jesaca,Mkapa na Kiwkete wamisha kaa wakakubaliana kuwa rais awe mwinyi na ndivyo alivyokuwa hata bara 2025 ndivyo itakavyokuwa hadi siku wakifa.
Hao ndiyo waliopiga kura juzi?! Mbona kura zimehesabiwa mubashara na wagombea wenyewe, Mkapa ,Jk, Mzee Mwinyi wala hawakupiga kura! Naomba tuwe wakweli.
 
Muungano ujilinde wenyewe kwa mema uyafanyayo sio ulindwe na watawala kwa Vitisho na mabunduki.
Mimi hadi leo sijawahi ona umuhimu wa huu muungano.
Kuna manufaa gani watawala wanayapata katika huu muungano kweli? Wananchi tunanufaika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…