Kama ni kipyenga tayari kimekwisha pigwa. Mtizamo wa serikali unajulikana kama ulivyo kwa sasa wa CHADEMA.
Hadi sasa haipo tarehe wala uelekeo wa lini Rais anaweza kukutana na Chadema kama chama.
Ni wazi kuwa msimamo wa serikali haukuwa wa bahati mbaya. Ambapo hakukuwa na sababu ya kuunganishwa kwa mambo ya katiba mpya na masuala ya mikutano ya siasa ambayo ni mawili tofauti. Hii ikiwa hata kama palikuwa na nia njema ya kutaka muda zaidi kuhusu katiba.
Uwezekano mkubwa ni kuwa timu ya washauri hapa ni ile ile. Hakuna shaka nia ni kuendeleza ya mwendazake bila mwendazake.
Hawa yumkini ni sehemu ya wale waliokula yamini ya kumfarakanisha Rais na yeyote (na hasa Chadema) kwa lolote hata kama ni la kijinga:
Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa
Yumkini hawataruhusu mkutano wa Chadema ikulu. Wala hawataruhusu kuona Chadema inakaribiana na watanzania wengine.
Kutokea hapa ni vyema kujiandaa kisaikolojia na ki mikakati. "Vita ni vita Mura!"
Kutokea hapa, litegemewe tamko rasmi lenye maudhui ya kuibagaza na kuishtaki Chadema kwa wananchi. Kuwa wakati palikuwa na fursa ya mazungumzo, wao wamekwenda kuchukua hatua zao ambazo yumkini zitapotoshwa vilivyo.
Wananchi watafanywa kuamini kuwa Chadema ni kundi la wahuni linalopaswa kushughulikiwa kwa nguvu zote. Hapo ndipo ule utabiri utakapokuwa umetimia kuwa, "tutegemee hali iliyo mbaya zaidi hata kushinda kipindi kile."
CCM ni ile ile hivyo haisaidii kujisahaulisha namna yao ya makabiliano.