Binafsi Kwa hotuba ya Rais Samia naona ni yule yule wa Jana na Sasa situation itakuwa worse
1. Hotuba ya Rais Kwa maksudi haijakemea ufisadi na Rushwa.
Nadhani Cancer kubwa ya taifa hili ni ufisadi,
Matumizi mabaya ya pesa za umma zinaliwa na wachache.
Hii inasababisha hospital hazina madawa, shule hazina madawati n. K
2. Hajakemea cancer ya utekaji na mauaji holela ya Watanganyika.
Hili tatizo limeweka doa kwenye utawala wake maelfu ya Watanganyika wametekwa na wengine kuuliwa na wengi walikuwa wakoseaji.
Kwa hotuba ya Rais Samia kutokulizungumza hilo na kulikemea ni wazi vitendo hivi vitaendelea
3. Hajaongelea tume mbovu ya uchaguzi.
Zaidi sana amezidi kuisifia Kwa kumpa ushindi fake na kuiba kura.
Hajaongelea kuirekebisha, maana yake yeye anaona hii tume Iko sawa na hapo tutaendelea kuona tulipata viongozi walioiba uchaguzi
4. Rais Samia hajaongelea mchakato wa kupata Katiba mpya.
CCM wamekuwa wakitumia hii katiba mbovu ya mwaka 1977 kunyanyasa Watanganyika
Katiba mpya ndo inampa mamlaka Rais yasiyo na kikomo, kuleta ufisadi na kuzaa Mahakama isiyo huru na bunge dhaifu lisiloweza kumwajibisha serikali
5 Hotuba ilijaa shopping list
Karne hii Rais kutoa ahadi za diwani ni aibu
Hotuba ilijaa nitaleta hospitality, sijui vyoo, barabara , kujenga masoko ambayo ni mambo madogo
Rais ilitakiwa atamke sera na uwezeshaji
6. Kuanzisha Kwa wizara maalum ya vijana
Binafsi nampongeza Kwa wazo hili
Vijana wa kitanzania wana changamoto nyingi na ndo wengi
Wizara hii ikupewa bajeti nzuri ikawezesha ajira, kilimo chenye tija, safari, sanaa n. K itasaidia Gen z wetu wengi
Naona Rais hana majuto Kwa yaliyotokea anaona Watanganyika ni kama hawajajielewa
Sisi tunataka
1. Katiba mpya
2 Tume huru ya uchaguzi
3. Uchaguzi urudiwe upya
4. Wote waliopewa kesi za uhaini Kisiasa waachiwe akiwemo Lissu na Niffer
5 waliotekeleza mauaji wa Watanganyika zaidi ya 10,000 wakamatwe na kufikishwa kwenye mahakama
5 Rais Samia awajibike Kwa kujiuzulu ili kulinda heshima yake aliyoijenga muda mrefu.