Pre GE2025 Tathmini ya Vyombo vya Habari kuhusu kuripoti matukio ya kisiasa nchini Februari 2025

Pre GE2025 Tathmini ya Vyombo vya Habari kuhusu kuripoti matukio ya kisiasa nchini Februari 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Kwa Mwezi Februari 2025, vyombo vya habari vilivyo vingi binafsi naona vimeendeleza kukibeba chama tawala huku vikigandamiza vyama vingine katika usawa wa kuripoti matukio ya kisiasa. Kuna baadhi ya vyombo kama Wasafi vilifikia kubrand magari yao kwa rangi za CCM, vilipohudhuria mkutano mkuu wa CCM uliompitisha Samia na Nchimbi kuwa wagombea Urais 2025

Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikilalamikiwa kwa kuegemea upande mmoja, hasa kwa kutoa nafasi zaidi kwa chama tawala, CCM, huku vyama vya upinzani hususani CHADEMA na ACT Wazalendo vikipewa nafasi ndogo katika taarifa zao.

Kumekuwa na matukio ya vyombo vya habari huru kama vile Jambo TV na Mwananchi Communications kukumbana na vikwazo kutoka kwa mamlaka, ikiwa ni pamoja kukamatwa kwa waandishi wao au kufukuzwa eneo la tukio ambapo upinzani wana jambo lao

Pamoja na shuruba wanazopitia, vyama vya upinzania vimeendelea kutumia majukwaa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii na vyombo huru vya habari, kufikisha ujumbe wao kwa umma.

Licha ya vikwazo, kumekuwa na mijadala huru katika Digital Platforms, ambapo wananchi na wadau wa siasa wamekuwa wakijadili kwa uwazi masuala mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

Ingawa kuna juhudi za baadhi ya vyombo vya habari kutoa taarifa zisizo na upendeleo, bado kuna changamoto kubwa katika kuhakikisha usawa wa kuripoti matukio ya kisiasa nchini Tanzania. Ni muhimu kwa vyombo vya habari kuzingatia maadili ya uandishi na kutoa nafasi sawa kwa vyama vyote vya siasa ili kuchangia katika demokrasia yenye uwazi na haki.

Pia soma > Pre GE2025 - Hali ya Vyombo vya Habari kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025: Kuna uhuru wa kutosha katika utekelezaji wa majukumu yao?
 
Back
Top Bottom