SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Katika hatua ya robo fainali ya mashindano ya CAF Shirikisho, Simba enaenda kukutana na timu mojawapo kati ya hizi tatu, Stellenbosch ya Afrika Kusini, ASEC Mimosas ya Ivory Coast na Al Masry ya Misri.
Hii ni tathmini yangu fupi ya timu hizi tatu na aina ya upinzani ambao Simba iutegemee.
AL MASRY
Simba ilifahamu fika kuwa itaenda kukutana sana na timu za waarabu msimu huu na ni kitu ambacho inabidi ujifunze kukikabili katika mashindano yote ya CAF maana kawaida ndiyo timu ngumu.
Simba kwa kujua hilo iliweka kambi yake ya pre-season nchini Misri. Hii ilisaidia kuwaandaa wachezaji mapema sana kujua kikwazo kikubwa cha msimu ni kipi katika kufikia malengo ya klabu.
Kama ilivyotarajiwa, hatua ya awali kabisa Simba ikakutana na kigingi kizito cha Al Ahly Tripoli ya Libya, ikavuka tena kwa kishindo. Hatua ya makundi ikakutana na waarabu wawili Sfaxien ya Tunisia na CS Constantine ya Algeria, simba ikashinda mechi 3 kati ya 4 na timu hizo ikiwemo kuweka rekodi ya kumfunga mwarabu nje ndani. Maandalizi ya pre-season kujiandaa na waarabu yakaonesha kulipa mpaka sasa.
Sasa kuna uwezekano wa kukutana na huyu mwarabu mwingine hatua ya robo fainali. Kutoka sasa kama Simba itafika hadi fainali kuna uwezekano mkubwa wa kukutana na waarabu wengine wawili au watatu. Nadhani hili lilifikiriwa mapema sana na Simba imejiandaa kwa hilo.
STELLENBOSCH
Hii ni timu ambayo imeanza kutingisha siku za hivi karibuni. Mwanzoni kwa msimu huu Mo Dewji aliitembelea hii klabu na kuisifia. Ni wazi Mo na Simba walishanusa potential ya hii timu kabla hata wengi hawajaijua au kuitilia maanani.
Ni timu ya kuizingatia sana maana imeonyesha imedhamiria kuja kuleta ushindani ndani ya ligi ya Afrika Kusini na Afrika kwa ujumla.
ASEC MIMOSAS
Kwa msimu huu ASEC ina timu ya kawaida sana ila kitendo cha kufika robo fainali kinaonyesha siyo timu ya kubeza. ASEC haikaukiwi vijana wenye njaa ya mafanikio na usije kushangaa mwishoni mwa msimu huu wakatoa mastaa wengine wapya kabisa.
Wasiwasi wangu mkubwa kwa ASEC kulinganisha na hizo timu zingine zinazoweka kukutana na Simba ni kuwa Yanga inaweza kuweka mkono wake kuzipa ugumu mechi za Simba iwapo itakutana nayo. Yanga ikumbuke kuwa ASEC ni moja ya timu 4 zinazoweza kuishusha Yanga kwenye rank za CAF kwa jinsi zinavyoendelea kufanya vizuri kwa hiyo wakiisaidia watakuwa wanajishusha wenyewe!
Kingine kinachonipa moyo ni kuwa ASEC inaendeshwa kiprofesheno na ina mahusiano mazuri ya kibiashara na Simba. Sitegemei kama wataingia kwenye hizo siasa za Simba na Yanga. Nadhani wakikutana na Simba watakuja kucheza mpira wa fair tu usio na drama zozote.
Kwa kumalizia, huu ni utabiri wangu wa matokeo. Nategemea yoyote atakayekutana naye, Simba itavuka kwenda nusu fainali.
UTABIRI:
Al Masry - Simba itashinda mechi zote mbili, nyumbani na ugenini
ASEC - Draw ugenini, Simba inashinda nyumbani.
Stellenbosch - Draw ugenini, Simba itashinda mechi ya nyumbani.