Tathmini yangu kwa mwelekeo wa elimu ya tanzania.

Dornatero

Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
15
Reaction score
8
Habari watanzania wenzangu. Ni majuzi tu Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ilitoa matokeo ya kidato cha nne. Sipendi kurudia tkwim zake mana zinachefua. Tathmini yangu ni juu ya wapi tulitoka, wapi tulipo na wapi tunaelekea. Nachochukkizwa nacho mimi ni tathmini ya matokeo na majibu yasiyokua na tija yaliyotolewa na wizara. Swali la kujiuliza ni je? Tulilazimishwa kufungua shule nyingi pasipo na tathmini ya waalimu? tulilazimishwa kujaza wanafunzi madarasani pasipo na kujua uhaba wa miundombinukama maktaba na vitabu?
Nakumbuka enzi ya miaka ya 1990 tulikua na shule za binafsi na shule za serikala. Hapa ilitupasa kua na wastani wa kutosha ili kuingia sekondari. Pia kuliandaliwa mnyororo wa masomo mwanafunzi aliyefanya vizuri masomo ya sayansi alijua kabisa ataenda shule za sayansi au vyuo vya ufundi, hali kadhalika wale wanaofaulu masomo ya biashara walijua Shaikom ndio ndoto yao. Hii ilitoa fursa ya mwanafunzi kua na tamaa ya kufanikiwa kimasomo na kuirahishia serikali mgawanyo wa rasilimali kama wataalam(waalimu), vitendea kazi na usimamizi bora wa taaluma mashuleni.
Leo hii kila kata inalazimishwa kuwa na shule ya sekondari bila kuangalia tofauti ya kipato cha wazazi wa kata husika na kukumbuka kua tunawanyima watoto fursa ya kupanua ufikiri katika mazingira. Lazma ifikie hatua tukubali kua sote kama jamii ya Watanzania tunahusika kwa matokeo haya mabovu ila serikali iliyo na dhamana ya usimamizi wa nchi pia ikubari kuanza upya mchakato wa kujua dhima ya kua na shule nyingi.
Tusipokua tayari kukubali makosa tunakoelekea ni kubaya zaidi, haiwezekani nchi inakua na wajinga wengi kuliko wasomi na bado tukadai tuko katika harakati za maendeleo.
TUMEVURUNDA TUJIPANGE UPYA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…