Tatizo gani hili msaada plzzzzzz

Manselly

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2010
Posts
456
Reaction score
130
Habari wadau
Mimi ni jinsia ME na umri 27
Nasumbuliwa na tatizo la tumbo kuchafuka na kichefu chefu kikali. Kila asubuhi mara nyingi tumbo linachafuka hapo naweza jiskia kwenda haja nikienda natoa kitu kama mapovu tu au naharisha hali inayoendelea mpaka ntakapotapika ndo linarudi katika hali ya kawaida.
Mwanzoni nilizani labda ni minyoo nimemeza albendazoe wapi nikatumia tiba asili ya kitunguu swaumu(according to Mzizimkavu) lakini wapi hali ya kichef chef na kuvurugika inapotokea hospital wakanishauri nitumie dawa flan yaitwa Nosic wapi no changes.
Nipo dilema hata cjui ni tatizo gani hebu nishaurini nikapime nn labda au nianzie wap hili tatizo.Naomba jopo la wataalam tafadhali mnisaidie
 
kwa ushauri nenda hospital ukapime waweza stool (faeces) utapata jibu mkuu waweza kuwa na minyoo.
 
Ujue sijui kwann yani watu tukiwa wazima tunakua na jeuri sana.Tunasahau kwamba hili sio jukwaa la utani ni watu makini wanajadili mambo makini mbonaadmn ameweka page ya utani/jokes tunaiacha tunaleta utani humu
 
Pole sana nenda hospitali ukapime, kuna sababu nyingi zinaweza kusababisha hilo tatizo,
 
Inaeza kuwa ulcers (vidonda vya tumbo ) pia kaka......used to have such symptoms...nikienda kupima naambiwa mara amoeba...mara minyooo lakini shida ilikuwa ulcers....nikaandikiwa dawa inaitwa Heligo Kit sijaumwa tumbo wala kupata maumivu tangu mwaka 2009..
 

Haya ndo mambo mimi nataka.Nambie mkuu ulienda hospal gan au kwa docta nani niende na walikupima nini na nini?
 
Tumia Dawa zangu hizi mojawapo kisha uje hapa unipe Feedback.

Asali safi mbichi ya nyuki wakubwa, imetambuliwa kwa kipindi kirefu kama dawa ifaayo kuondowa mchafuko wa tumbo pamoja na kichefuchefu, kwa hiyo tengeneza chai kisha tia kwenye kikombe asali vijiko vinne na unga wa mdalasini vijiko viwili koroga tumia, kesho yake vile vile fanya hivyo utapata nafuu kubwa sana Inshaallah.

Dozi nyingine ya ugonjwa huo, twanga kamun aswad unga wake uwe ujazo wa kikombe cha kahawa, kisha kamua machungwa makubwa 6, juice yake weka kwenye chupa. mgonjwa atatumia kikombe cha kahawa 1x2 wiki moja.

Dozi nyingine ni Dawa inayoitwa (Algama) mpingadume-muubuzi na tangawizi mbichi twanga sawa sawa kisha chemsha dawa hizo ujazo wa maji nusu lita.Mgonjwa atatumia nusu kikombe 1x1 siku 6. tahadhari mama mjamzito asitumie dozi hiyo ni hatari
 

Ni PM nikupe dawa kijana.
 
Sasa mi nashangaa unajisikia vibaya hivyo harafu unakimbilia jf kupata dawa za comment.
 
Haya ndo mambo mimi nataka.Nambie mkuu ulienda hospal gan au kwa docta nani niende na walikupima nini na nini?

Jaribu kuacha baadhi ya chakula kwa mda wa wikiwiki. Mfano wali wiki je tatizo ilo unalisikiaje kama bado hacha chengine mpaka utakuwa sawa
Tatizo langu halikuwa kama lako ila mimi magesi kuara mlenda nimekula madawa mapaka basi sasaivi safi na punguza kula. Chakula kingi nyakati za usiku
 
Ukienda haja kubwa unatua vitu vyeupe!!?.......isije ikawa....anyway..

Nenda hospitali kwa msaada zaidi. Pole sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…