Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,180
- 7,346
Alishawahi kusema mwenyewe na jana Dr Slaa kakumbushia kuwa RA ana kipato cha zaidi ya Tsh Billion 240 kwa mwaka!Hii ina maana kuwa RA anaingiza faida ya zaidi wa Tsh million 657 kwa siku!
Naomba kuuliza hizi fedha anazipeleka wapi? RA na mabilionea wengine hata Tanzania, fedha zao wanapeleka wapi? Sijawahi kusikia RA kafadhili kitu chochote kikubwa katika jamii ya Watanzania. Ukiacha vimichango vidogo kama million 3 alizowahi kumpa Mtikila, na kwingineko, RA anapeleka wapi fedha zake? RA ana charity fund/foundation yoyote Tanzania?. Tunasikia mabilionea wa nchi nyingine wanachangia kujenga mahospitali, wanatoa mahela mengi kwenye taasisi za utafiti n.k. (eg Bill and Melinda Gates foundation). Mabilionea wa Kitanzania kama RA, hela zao zinaenda wapi?
Tukisema kuwa zinafadhili ugaidi duniani, au zinafadhili vita sehemu fulani, au zinaendesha serikali kandamizi sehemu fulani, au ziantumika hapa hapa kufadhili makundi, njama na mipango hatarishi kwa maslahi ya watu fulani, tutakuwa tunakosea? Hivi si kuna FBI na sheria ya ugaidi ilishapitishwa Tz? Kama vyombo vyetu vya usalama haviwezi kufuatilia mambo kama haya, kwa nini hivi vya kimataifa visiingilie na kuhakikisha fedha hizi hazihatarishi usalama wa dunia?