Tatizo kwenye Kitovu

Tatizo kwenye Kitovu

Blaki Womani

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2011
Posts
11,229
Reaction score
13,442
Habari ya leo JF

Ninatatizo la kitovu kutoa maji kwa muda mrefu sasa miaka 25 nimekwenda hospital bila mafanikio nimemwona mtaalamu wa ngozi KCMC kipindi cha nyuma lakini kwa sasa nimekata tamaa.

Sio kwamba kinatoa maji muda wote bali pale ninapotumia dawa na kufanyiwa dressing kinapona naweza kukaa muda hata wa miaka miwili bila kutoa maji halafu kinaanza kutoa maji mara ya mwisho hospital niliyokwenda Dr. aliniambia inawezekana kilikatwa vibaya ndio inasababisha wakati mwingine kuwa hivyo.

Naomba kwa anayejua namna ya kusaidia tatizo hili kuondoka kabisa anisaidie.
Asante.
 
Pole sana - Huwa sina Imani na Madaktari na ndiyo maana natumia zaidi dawa za kienyeji!
 
Dawa gani ya kienyeji

BW kwanza pole sana kwa tatizo, ni kweli matatizo mengi ya kitovu sijawahi sikia mtu amepona kwa dawa za hospitali, mengi yanaponeshwa na dawa za kienyeji, ni kweli tatizo lako linasababishwa na kitovu kukatwa vibaya, niliwahi kumwona mtu ana tatizo kama hilo, dawa aliyotumia ilinishangaza kidogo, alichukua kipande cha gunia na kukichoma kwenye jiko la mkaa, kilivyoungua akakitoa na kusaga ili apate powder, then akawa anatia kwenye kile kitovu, kilichotokea sikuamini kwani tatizo lilimalizika ndani ya siku 7.

Unachoma hicho kigunia kwenye moto usio mkali ili kisiungue chote. Pole again ndugu yangu.
 
SL
Nashukuru sana kwa hilo
niliwahi kuagiziwa dawa nyingine nikaange miwa jikoni mpka yawe majivu
niweke kwa muda wa siku saba nitapona nilifanya hivyo kweli kiliacha kabisa
kutoa maji lakini baada ya miaka 3 ilirudia tena,
ninakwenda kulifanya kama ulivyoniambia maana nina mwezi sasa kinatoa maji
Asante
 
POLE SANA BW,
Natamani sana ningekuwa na uwezo wa kukutibu au hata kumfahamu mtu anayeweza kukutibu,
lakin bahati mbaya sifahamu na simjui yeyote,ila NAAMINI KUPITIA JF unaweza kupata ufumbuzi wa tatizo lako.
POLE SANA.
 
Pole sana BW.... nahisi maumivu yake hayaelezeki. Hebu tusikie wataalam hapa watasemaje.
Habari ya leo JF

ninatatizo la kitovu kutoa maji kwa muda mrefu sasa miaka 25
nimekwenda hospital bila mafanikio
nimemwona mtaalamu wa ngozi KCMC kipindi cha nyuma lakini
kwa sasa nimekata tamaa
Sio kwamba kinatoa maji muda wote bali pale ninapotumia dawa na kufanyiwa dressing
kinapona
naweza kukaa muda hata wa miaka miwili bila kutoa maji halafu kinaanza kutoa maji
mara ya mwisho hospital niliyokwenda Dr. aliniambia inawezekana kilikatwa vibaya ndio
inasababisha wakati mwingine kuwa hivyo
naomba kwa anayejua namna ya kusaidia tatizo hili kuondoka kabisa anisaidie
Asante
 
Asanteni wanaJF wote
naamini kwa sala zenu ipo siku nitapona
 
Pole mkuu Mungu atakuwezesha upate kupona.
 
Jamani nina tatizo la kuvuja maji kwenye kitovu.... Naomba kujua tatizo hili linasababishwa na nini..
 
Habari za jioni wakuu... Nina tatizo tajwa hapo juu na sijui limesabishwa na nini
 
limekuanza ukubwani au ulikuwa nalo tangu utotoni...?
na vipi emeenda hospital?
 
Back
Top Bottom