Pole sana Farida. Tatizo lako linaweza kusababishwa na mambo mengi. Mojawapo ni hormone zako kutokuwa katika viwango vinavyofaa kwa wakati muafaka (hormonal imbalance). Ila kama ulivyosema, linaweza kutokana na matumizi ya hormones za kuzuia mimba (contraceptives). Kutokana maelezo yako inaonekana matatizo yako yalisababishwa na hizo sindano. Kwa kawaida, inategemewa mama apate uja uzito kati ya miezi 6-12 baada ya kuacha sindano. Sasa kama mfumo wako wa hormones umeshindwa kurudi kwenye hali ya kawaida kiasi cha kutopata uja uzito basi jaribu kumwona Doctor ambaye akishachunguza hali yako kwa makini anaweza kukupa matibabu ya hormones nyingine ili kukurudisha kwenye hali ya kawaida.