nilikuwa nimechoma sindano ya kuzuia ujauzito mwaka jana mwezi wa tano. ila nikawa naenda breeding kwa muda wa miezi mitatu bila kusimama. baada ya hapo siku zikabadirika kwa mwezi ninakuwa nina breed mara tatu. na siwezi kushika ujauzito ninataka kujua je ninatatizo gani.
Samahani naomba usahihishe. Unaongelea bleeding au breeding? Hivi ni vitu viwili tofauti. Bleeding ni kutokwa damu wakati breeding ni mambo yanayohusiana na kuzalisha viumbe mfano mimea au wanyama kwa kutumia wazazi wa koo (breeds) tofauti ili kupata chotara ambao wana sifa na ubora zaidi ya wazazi wao. Wafugaji wa ng'ombe wanajua vizuri mambo ya Friesian anavyokuwa bomba akitengeza chotara kwa kupandishwa kwa ng'ombe wa kimasai. Hii inanikumbushwa mwalimu wangu aliyemwambia jamaa kuwa makini kwani alikaribia kuchanganya election na erection!!
Sasa hata kama kasema breeding tuseme hukumuelewa? nadhani kama unafahamu kiswahili usingeshindwa kuelewa kamaanisha nini? kama wewe ni Mtanzania unajuwa wazi kuwa matamshi ya herufi 'L' na 'R' yanawapiga chenga wengi, isiwe sababu ya kuanza tasnifa.
Wewe ulitakiwa umwambie kakosea spelling sio sijui wafugaji friesian........ Grrrrrrrrr!
tatizo la kutokwa damu ya uzazi bila mpangilio ambalo lina sababisha nisiweze kushika mimba.
Pole sana Farida. Tatizo lako linaweza kusababishwa na mambo mengi. Mojawapo ni hormone zako kutokuwa katika viwango vinavyofaa kwa wakati muafaka (hormonal imbalance). Ila kama ulivyosema, linaweza kutokana na matumizi ya hormones za kuzuia mimba (contraceptives). Kutokana maelezo yako inaonekana matatizo yako yalisababishwa na hizo sindano. Kwa kawaida, inategemewa mama apate uja uzito kati ya miezi 6-12 baada ya kuacha sindano. Sasa kama mfumo wako wa hormones umeshindwa kurudi kwenye hali ya kawaida kiasi cha kutopata uja uzito basi jaribu kumwona Doctor ambaye akishachunguza hali yako kwa makini anaweza kukupa matibabu ya hormones nyingine ili kukurudisha kwenye hali ya kawaida.