Tatizo la Elimu yetu ni kwenye shule za Umma siyo za Binafsi

Tatizo la Elimu yetu ni kwenye shule za Umma siyo za Binafsi

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Kwenye mfumo wa Elimu Yetu tuna matatizo mengi sana ambayo kwa haraka haraka inawezekana ikatuchukua hata miaka zaidi ya 20 kuyarekebisha, tena kama tukiwa makini na tuliodhamiria kufanya marekebisho yanayotakiwa.

Kwenye Mfumo wetu wa Elimu watu waliofundishwa kuwa Maafisa Elimu kwenye vyuo vyetu vikuu, kutokana na ukosefu wa ajira ndiyo wanageuka kuwa waalimu kwenye shule zetu za Msingi na Sekondari. Mtu aliyeandaliwa kwa miaka mitatu au zaidi kuwa msimamizi wa Sera za Elimu, mitaala, na usimamizi wa mifumo ya Elimu ndiyo wanakuwa mwalimu.

Kwenye mfumo wetu wa Elimu Kanuni na Taratibu za kuendesha elimu zinashangaza sana. Elimu ambacho ni kitu muhimu sana kwa Taifa kama ulivyo moyo kwa viumbe hai, imeachwa mikononi mwa mtu mmoja tu, WAZIRI WA ELIMU.

Waziri wa Elimu anaweza kubadili mitaala ya shule, mfumo wa kusoma (Idadi ya madarasa), mfumo wa kusahihisha, idadi ya masomo mashuleni, mifumo ya ajira na nafasi za uongozi kwa waalimu, bila ya kuingiliwa na mtu yeyote yule.

Matokeo yake Elimu yetu imekuwa na mabadiliko kwa kadri Waziri wa Elimu aliyeko madarakani anavyoona inafaa. Siyo Bunge wala Rais aliyemteua waziri wa Elimu wanaweza kugeuza maamuzi yanayotolewa na Waziri wa Elimu. Matokeo yake Elimu yetu hutegemea zaidi Kudra za Mwenyezimungu kumjaalia "Hekima" na "Busara" waziri wa Elimu atakayekuwa madarakani kwa wakati husika.

Ukienda kwenye mashule ya Umma utashangaa ndiko kanuni za kuendesha shule hazifuatwi kabisa. Kanuni za wanafunzi darasani inataka wanafunzi wawe wanafunzi 45 kwa kila darasa. Lakini kwenye shule za Umma darasa moja linakuwa na zaidi ya watoto 100 kwa wakati mmoja.

Kwa mujibu wa Kanuni za Elimu angalau kwa kiwango cha chini kabisa Kitabu kimoja cha Kiada, kinatakiwa kitumiwe na watoto si zaidi ya wawili au kwa watatu kwa kiwango cha juu kabisa. Nenda sasa kwenye shule za Umma ukute darasa zima lenye watoto 100 lina vitabu saba tu vya kiada kwa somo husika.

Kwa ngazi ya shule za Sekondari nako hali siyo nzuri hata kidogo. kwa ivo kwa Tanzania Tatizo la mfumo wa Elimu linaonekana zaidi kwenye shule za umma na siyo kwenye shule za Binafsi.
 
Mkuu, kwenye shule za umma imebakia kuwa kiki za kisiasa ili kuwapa umaarufu watawala. Lakini katika shule binafsi ni sehemu ya biashara yenye matakwa ya kujiendesha kibiashara, na kiendelevu kupitia matokeo ya kiushindani.

Utoaji wa elimu bure ni suala la kukidhi haja ya "supply driven" kwa vigezo vya kisiasa, lakini kwa ugharamiaji wa elimu kwa mtu binafsi kwa sekta binafsi ni "demand driven" kwa vigezo vya haha ya ubora wa huduma inayohitajika.
 
Hupo sahihi facilities hazitoshi Pamoja na hayo Mimi sioni umuhimu wa kuwepo Elimu bure ambayo mwisho wa siku wanafanikiwa wachache

Naomba Serikali waweke Ada katika Elimu hata Kama itakuwa 20k kwa mwaka hila mwisho wa siku tutapata facilities za kufundishia kwa kiwango fulani

I was been there shule X ya secondary kiufupi unaweza kutoa machozi ukiangalia watoto wanavyosoma .

Elimu bure ingewekwa chuo kikuu na siyo huku chini

Serikali inatoa Elimu bure lakin. Without any Arrangement
 
Leo Waziri wa Elimu anataka kufuta Darasa la Saba. Lakini watanzania wengi hawajawahi kuuliza ilikuwaje darasa la nane likafutwa na tija yake mpaka sasa ni nini? Kama la nane lilifutwa na kubakizwa madarasa saba kwa Elimu ya Msingi. Tuambiwe hayo saba tena kuna tatizo gani limetokea hadi yabaki sita??
 
Bro, haya mambo kiukweli ukiyatafakari sana...unaishia kuumia mwenyewe tu.

Hao viongozi wala hawana muda wa kumpa elimu bora mtoto wa maskini kwa sababu hiyo ndo kiki inayowafanya waendelee kubaki madarakani....

Wajinga wakiwa wengi, wao viongozi ndo wanafurahi kwa sababu hakuna wa kuwahoji juu ya utendaji wao na hawana hofu ya kuondolewa madarakani....

Acha tuendelee kuwa shamba la bibi kwa kuwa wananchi wenyewe tunafurahia kuitwa wanyonge
 
Bro, haya mambo kiukweli ukiyatafakari sana...unaishia kuumia mwenyewe tu.
Hakuna jinsi ya kuyabadili??

Au kila mtanzania asiye madarakani ni mnyonge anayesubiri kunyongwa ili apewe haki yake ya kuzikwa??
 
Hupo sahihi facilities hazitoshi Pamoja na hayo Mimi sioni umuhimu wa kuwepo Elimu bure ambayo mwisho wa siku wanafanikiwa wachache .

Naomba Serikali waweke Ada katika Elimu hata Kama itakuwa 20k kwa mwaka hila mwisho wa siku tutapata facilities za kufundishia kwa kiwango fulani.

I was been there shule X ya secondary kiufupi unaweza kutoa machozi ukiangalia watoto wanavyosoma .

Elimu bure ingewekwa chuo kikuu na siyo huku chini

Serikali inatoa Elimu bure lakin. Without any Arrangement
I was been there..?????!!!!
Sema, I have been there...✓
 
Leo Waziri wa Elimu anataka kufuta Darasa la Saba. Lakini watanzania wengi hawajawahi kuuliza ilikuwaje darasa la nane likafutwa na tija yake mpaka sasa ni nini? Kama la nane lilifutwa na kubakizwa madarasa saba kwa Elimu ya Msingi. Tuambiwe hayo saba tena kuna tatizo gani limetokea hadi yabaki sita??
Nia yetu yabaki manne tu. Ili mfumo wetu wa elimu uwe 4:4:2, 4 primary, 4 sekondari na chuo kikuu badala ya 3 iwe 2 tu.

Kama qt imewezekana, kwa nini huo mfumo pendekezwa ushindikane?
 
Back
Top Bottom