Habari njema kwa watanzania hususan wenye magonjwa ya figo Hospitali ya Trauma centre and Well Woman Clinic ilipo masaki imeshazindua rasmi matibabu ya usafishaji wa damu kwa watu wenye matatizo ya figo,matibabu haya kwa kipindi kirefu yalikuwa ni vigumu kupatikana nchini kutokana na mitambo hiyo kupatikana kwenye Hospital chache sana hapa nchini na kulazimu baadhi ya watanzania kutumia gharama kubwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibu hayo.
Ni fursa pekee kwa watanzania kutumia vyema bahati hii kwani mbali na matibabu haya pia kuna huduma na mitambo ya kisasa katika kila idara vikiwemo Digital mammography, Dexa unit ni mtambo pekee Tanzania nzima ambao hupima na kugundua kiasi cha Calcium ,ambayo huimarisha mifupa kwani upungufu wake husababisha maumivu mwilini na hupelekea hata kuvunjika kwa Hip Joint (yaani nyonga kwa Kiswahili).
Watanzania tutembelee Trauma Centre iliyopo Masaki mwisho inatizamana na Coral Beach Hotel.