Tatizo la gari kutoa moshi mwingi na mzito

Tatizo la gari kutoa moshi mwingi na mzito

BRO SANTANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2015
Posts
1,845
Reaction score
2,248
Heshima kwenu wakuu.
Nina gari yangu aina ya toyota runx.
Juzi kati iliingia kwenye shimo kwa mbele na kuinama sana huku upande wa nyuma ukiwa juu.
Sasa baada ya kutolewa ikawa inatatizo hilo ka kutoa moshi mzito kwenye exhasault(bomba la moshi)
Sasa leo nimefungua bonet na kucheck ile sponji inayochuja hewa nikakuta imeloa oil ni balaa.
Msaada wakuu nifanyeje hapo lkn tatizo lilianza kabla ya gari kuingia shimoni na baada ya kuingia shimoni ndio tatizo limeongezeka.
 
Mkuu peleka kwa wataalam haraka wakalichunguze,hamna namna nyingine hapo!
 
hapo itakuwa baada ya gari kubinukia mbele oil itakuwa imemwajika kwenye sehemu ya juu ya engine,mara nyingi ikitokea hivi gari huwa linazima lenyewe ili kuizuia engine isiharibiwe since oil presure inakuwa ndogo sana,iwapo utaendelea kulilazimisha gari kuwaka itapelekea kwenye kitu kinaitwa "hydrolock" na engine itakuwa ndio byeee...

Unachotakiwa kufanya ni kufungua hiyo top na kuondoa plugs na kuzisafisha pamoja na kuondoa oil yote iwapo imeingia kwenye mojawapo ya cylinder,unafanya hivyo baada ya kuzungusha engine kwa mkono na kurusha oil yote nje:warning wakati unafanya hii kitu weka mbali uso wako.baada ya hapo safisha oil yote iliyoingia kwenye cleaners n.k,then weka oil tena vizuri alafu piga moto gari nenda mbali kadiri uwezavyo,after 3 or 4 days utaona gari imerudi kwenye mstari.
 
Mkuu peleka kwa wataalam haraka wakalichunguze,hamna namna nyingine hapo!

Anajua wataalamu wapo humu JF ndio maana hajasita kuitumia hii fursa,kwenda kumuona mtaalamu mmoja ni tofauti na kuwaona wataalamu wengi kwa pamoja.
 
Anajua wataalamu wapo humu JF ndio maana hajasita kuitumia hii fursa,kwenda kumuona mtaalamu mmoja ni tofauti na kuwaona wataalamu wengi kwa pamoja.
Kweli kabisa mkuu.
Jf ni kila kitu nawashukuru sana kwa mawazo yenu
 
Back
Top Bottom