Tatizo la Gonjwa la Sukari (Diabets Mellitis): Fahamu chanzo, aina na ushauri wa tiba ya tatizo hili

Kongosho likiharibika unakufa ndugu. Sema Kongosho lina sumu sio kuharibika. Kongosho lina sumu na uchafu ukisafisha hilo kongosho umepona maradhi yako ya Kisukari. Sikiliza hiyo Video kuhus kongosho.
 
Mkuu naomba maelekezo ya ziada kidogo. Hiyo juice iwe plane yani isiwe na sukari? na je iwe nzito kwa maana ya kali au nyepesi mzimuo wa maji uwe mwingi?
.........Plane = Plain....
 
Ukwaju ? Tupe mechanism jinsi unavyosaidia kwenye mtu mwenye kisukari.
 
Wagonjwa wa kisukari njooni tujifunze, make huu ugonjwa ni tishio
 
Mimi nina kisukari natumia metformin. Nafuata diet,ninaamini nitaishi na kuona watoto wa vitukuu wangu. Achana na dawa za kienyeji. Usiwasikilize hawa wauza madawa yasiyopimwa viwango. Utaua figo zako bure.
Hakika umenipa moyo, nilikata tamaa juu ya huu ugonjwa. Kwasasa natumia metfomin, pia nmeanza diet, natumia ugali wa ngano nyeus, mkate wa ngano nyeusi kwa wanga, mboga za majani ndiyo chakula changu. Japo sukari kwasasa leo ipo juu sana. 18 hapo nilipima kabla sijala baada ya kula 20.5. Hakika itashuka
 
Mimi nina kisukari natumia metformin. Nafuata diet,ninaamini nitaishi na kuona watoto wa vitukuu wangu. Achana na dawa za kienyeji. Usiwasikilize hawa wauza madawa yasiyopimwa viwango. Utaua figo zako bure.
Tangu umegundulika ni mda gani..
 
18 hapo nilipima kabla sijala baada ya kula 20.5. Hakika itashuka
- Ni vyema ukafika hospitali, kama uko Dar nenda amana kuna dakitari mzuri wa kisukari , 18 - 20 ni kiasi kikubwa sana.
- Kuna uwezekano akakubadilishia dawa, ili kushusha na kuhakikisha haipandi kiasi hicho na kutoa ushauri zaidi jinsi ya kukabiliana na kisukari.
- Siku ya kliniki ya sukari Amana ni siku ya Jumatatu na Alhamisi.
 
Asante sana ndugu kwa kunishauri, nipo mkoani.
Hapa nmetoka hospital nna siku tatu, nililazwa kwa mda wa mwezi mzima, hivyo nimetoka kutumia insulin na kuja kwenye vidonge.
Binafsi naona ina shuka sasa, japo nahitaji zaidi kuishusha.
 
Acha stress mimi nimeikubali hali. Dr watu aliniambia kisukari sio adhabu. Kufuata masharti na dawa. Kupima mkojo ili kujua figo kama zipo Ok,kumuona cardiologist mara moja kwa mwaka,kupima Cholestérol mara moja kila miezi mitatu. Mkojo pia ni mara moja kila miezi mitatu. Kumuona optamologist mara moja kwa mwaka. Some time naiba nakula ugali. Kisukari sio adhabu cha muhimu kuacha masukari ya viwandani.
 
Kazana mazoezi na milo itashuka,mimi inanisumbua kipindi Cha ujauzito wanaita gestational diabetes nkijifungua inaisha though nimeshazoea ulaji bora hivyo naendelea nao tu
 
Kazana mazoezi na milo itashuka,mimi inanisumbua kipindi Cha ujauzito wanaita gestational diabetes nkijifungua inaisha though nimeshazoea ulaji bora hivyo naendelea nao tu
Asante sana, ninajitahid hilo
 
Utakaa sawa sisi tuna miaka mingi na huo ugonjwa fuata masharti tu basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…