ameline
JF-Expert Member
- Jan 8, 2013
- 2,292
- 1,151
Salaam ndugu zangu,. naomba msaada kwa anayejua matibabu ya keloids(uvimbe fulani mweusi huota kifuani, shingoni, mgongoni au hata usoni) kuna mdogo wangu |(wa kike)ana uvimbe huo nitaweka picha kama haitaeleweka, ana miaka kumi sasa akiwa na tatizo hilo, upo kifuani kila nikimpeleka hosp, doct anamwambia akizikata zitaota tena, labda twende KCMC ndipo tutapata madoctor wazur wanaokata na kuchoma, au anaweza kuziacha tu hazina madhara yeyote, wakati yeye anasema zinawasha wakati mwingine zinachoma kama sindano na zinaongezeka ukubwa.Sasa tupo dillema sijui nifanyeje ndugu zangu. ni kweli akikata hazitarudi? au tiba yake hasa ni nini au kama kuna mdau ambaye ameshawahi kuziondoa anishuhudie jamani maana naona hii kitu imemuathiri kisaikolojia kabisa huyu binti Ahsanteni