Tatizo la ' Kivuli '

FirstClass

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2016
Posts
1,100
Reaction score
1,363
Habari za wikend waungwana..

Kwa muda wa kama miezi2 nimekuwa muhudhuriaji wa hospitali kumuugiza Mama yangu Mzazi. Ndani ya miezi hiyo, amelazwa kama mara3. Tatizo linalomsumbua halieleweki. Anaishiwa na damu mara kwa mara, kelele masikioni. Miguu kuwaka moto. Ganzi miguuni. Baridi kali..

Sasa, majuzi alipokuwa amelazwa, kuna Mama flani aliniulizia kuhusu maradhi yanayomsumbua B Mkubwa. Nami nkamjibu ,bado nasubili majibu ya Maabara.

Yule Maza alishauri tucheki na tiba mbadala. Maana kwa anavyomuona yeye B mkubwa, kinachomsumbua si maradhi ya kawaida. Basi akanihaidi kunipa dawa zitakazo mpa ' Ahueni '. Bila malipo yani.

Kwa kuwa vipimo vya hospital havikubaini ugonjwa wowote. Niliomba kumtoa B Mkubwa hospitalini Pale. Tiba mbadala ikaanza rasmi.

Bda ya kama siku mbili, B mkubwa alianza kupata nguvu taratibu. Ikabidi nimtafute yule maza kumpa maendeleo ya mgonjwa.

Basi ikabidi nifunge safari hadi nyumbani kwa yule Maza, nilipofika alinistaajabu sana. Akasema ' Wewe pia unashida lakini hujielewi '

Hapa nilicheka kisha nikasema..' aisee mi hata kitanda cha hospital sijui radha yake. Sijawai kuugua ata maralia , sasa hiyo shida inakujaje. Acha utani aisee '

Yule Maza akanidadisi kisha akaniambia, hapana mi sjamaanisha hivyo ,akasema 'Huoni mipango yako mingi inafia njiani , huoni mambo yako mengi yanakwama. HUjawai kujiuliza?? '

Aisee kwa hili alinipatia kwa asilimia100.

Kishingo upande nikakubali. Nikasema ni kweli. Kwa hiyo nami ' nimelogwa? '

Akajibu hapana.. Hujalogwa. Kinachokusumbua ni ' Kivuli chako '

Uliwai kukanyaga madawa mabaya Njia panda, tatizo lilianzia hapo. Madawa yale yalifanya utofautiane na kivuli chako. Ndio kinachofanya uwe hivyo.

Hapa alinipa kitu kipya. Nikamwambia tumalize kwanza la B Mkubwa. Langu litafata nikiwa tayali..

Jf haijawai niangusha.
Kama ni kweli ninatatizo hili, n zipi njia salama za kujinasua. Kusali nasali sana tu.

Karibuni..
 
mh, m mbona nywele zimenisisimka ghafla, machale yamenicheza! aah hili tangazo
 
Ko anataka kukiosha kivuli chako sio!? Anyway ngoja mama apone alafu chenji ikibaki utampa amalizie kukisafisha kivuli chako maana kweli chenyewe kinaburuza chini ukitembea so lazima kiwe na muskheri
 
Unakwama wapi mkuu, km huna ukijuacho s unavunga tu aisee
Ko anataka kukiosha kivuli chako sio!? Anyway ngoja mama apone alafu chenji ikibaki utampa amalizie kukisafisha kivuli chako maana kweli chenyewe kinaburuza chini ukitembea so lazima kiwe na muskheri
 
Ushaingizwa kwenye ushirikina tayari .. na ukute una ma degree yako unakuja kutapeliwa na bibi anbaye hata darasa halijui
 
Ila hayo mambo ya upande wa pili yapo mbona sana mkuu, sometimes sio kila tatizo la kuchomwa sindano tu hospitali unaweza mpoteza mtu mihimu ohoo[emoji20]
Ushaingizwa kwenye ushirikina tayari .. na ukute una ma degree yako unakuja kutapeliwa na bibi anbaye hata darasa halijui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…