Mbali na mvua zinazoendela kunyesha kwa wingi,maeneo mengi ya Dar es Salaam mfano Changanyikeni (Chuo cha Takwimu, maeneo ya Kanisa Katoliki, Jeshini), Sinza na Kimara hayana maji kwa wiki ya pili sasa na hakuna taarifa yoyote kutoka kwa mamlaka zinazohusika.
Maji yanayouzwa yanapatikana kwa bei ghali ya sh. 1,500 paka 2,000 kwa ndoo (ukizingatia maeneo haya yanakaliwa na wanafunzi wengi, hali ya maisha inakua ngumu mno kuweza kumuda gharama za kununua maji kila siku).