Tatizo la kunuka mdomo(kinywa) husababishwa na nini?

Majoajosh

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2020
Posts
276
Reaction score
186


Wadau, heri ya mwezi mpya huu, nina swali ambalo linahitaji msaada wenu.

Kwa nini kuna baadhi ya watu midomo inatoa harufu mbaya!?

Hata Kama akipiga mswaki baada ya muda harufu hiyo hurudi.

Unakuta mtu meno ni meupe na masafi ila mdomo unanuka, shida ni nini?

Na dawa yake ni nini?

Karibuni wadau, shukrani sana.
*******

Ushauri



Pia soma: Ongezeko la watu kunuka mdomo

 

Sio kila kinachotoa harufu mdomoni kinahusiana na usafi wa kutokupiga mswaki, ukishafahamu hilo ndio utajua kwamba mwanadamu yoyote duniani lazima atoe harufu kinywani kwake. Kuna wengine wana matatizo ya kiafya tumboni pia.

Hili jambo ni gumu mno kulielezea, na ndio maana hata Dunia ya kwanza uuzaji wa Chewing gum, Spray za mdomoni zina soko sana, wewe ushangai mpaka wakina Obama wanatafuna Chewing gum, kunuka mdomo ni hasili ya mwanadamu aliepukiki hata, unaweza ukahisi unuki mwenzako akakusikia unanuka na unaweza kujihisi unanuka mdomo mtu mwengine asikusikie.

Kunywa maji mengi, na jaribu kila wakati mdomo wako uwe unachecheza kwa vitu vya ubuge ubuge,Kunywa maji kila mara na kutokuacha mabaki ya chakula kinywani usaidia pia kupunguza hali ya harufu.
 
Nilikuwa na tatzo km hilo nilielekezwa daw ya kusukutua kila nipigapo mswaki ni (mouth wash) nenda duka la dawa nunua Hydrogen peroxide itakusaidia km tatizo ni dogo
 
Nilikuwa na tatzo km hilo nilielekezwa daw ya kusukutua kila nipigapo mswaki ni (mouth wash) nenda duka la dawa nunua Hydrogen peroxide itakusaidia km tatizo ni dogo
Inauzwa kati ya 2000-2500 chukua leo itakusaidia
 
Samahan kwa mwenye thread...naomba niweke tatizo langu hapa wataalam wanisaidie manake ata kufungua uzi wangu siwez (new member)
**********
kwenu wataalam...mimi nasumbuliwa na kuwashwa ngoz..yan nkigusa kitu chochote kile ngoz inawasha sana na kuvimba...baada ya muda hurud katka hali ya kawaida...nmetumia dawa nyingi za hospital and mitishamba ila bado hali ni tete...msaada jaman 😪😪
 
Chukua uzi wa nguo, ingiza katikati ya meno chokonoa uone uchafu unaotoka.

Shida iko katikati ya meno. Utanishukuru baadae...

Hata upige vipi mswaki haitasaidia kama katikati ya meno uchafu haujatolewa kwa uzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna vile vijamaa vinaitwa tonsile stone aseee ni kipengeleeeeee. Namna ya kuvitoa achama mdomo chukua kioo kaa sehemu yenye mwanga wa kutosha kisha tumia cotton swabs au cotton buds kuviondoa.
 
Mkuu una allergy kuna dawa zipo mwone daktari.



Kua makini ukila chakula gani hio hutokea hlf uache kula kama hutaki kwenda hospitali.
 
Asante Sana boss
Nilikuwa na tatzo km hilo nilielekezwa daw ya kusukutua kila nipigapo mswaki ni (mouth wash) nenda duka la dawa nunua Hydrogen peroxide itakusaidia km tatizo ni dogo
Shukrani Sana boss
 
Wataalam Please njooni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…