jamani wana jf,hili jambo sasa naona limekuwa tatizo! ndugu yangu wa karibu kwa muda mrefu amekuwa na tabia ya kuongea huku akiwa katika usingizi mzito!yaani anaweza akaongea sentesi nzima kwa ukali au kwa upole,lakini akiamka halafu ukamweleza alichokuwa anaongea anakataa kabisa!mwanzoni tulizani ni utani au ndoto za utotoni lakini sasa hiv ni mtu mzima bado anayo hiyo tabia yaani hata usiku mnene anaweza akaongea tena anaweza hata kumtaja mtu jina katika maneno yake akimaliza anaendelea na usingizi! hebu naombeni mawazo yenu kama kuna mtu ana uelewa au uzoefu na jambo hili!