Tatizo la kupasuka mdomo

Tatizo la kupasuka mdomo

LAPUA MAGNUM 338

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2015
Posts
431
Reaction score
1,223
Habar wadau,

Nasumbuliwa na tatizo la mdomo kupauka sana na kuanza kupasuka pasuka kwenye lips kiasi kwamba ninapokula hata baadhi ya matunda kama nanas na chungwa napata sana tabu.

Nilijitahidi kupaka mafuta wakati wa kulala na asubuhi kukiwa na baridi lakini bado, Je kuna dawa naweza kutumia wadau, yeyote mwenye uelewa anisaidie.

Thanks!!
 
hakuna dawa hapo kama tatizo limekuanza tu ghafla hapo ni lishe tu, umekosa balanced diet. piga matunda na mbogamboga utaonaona linaisha lenyewe.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Huo ni upungufu wa Vitamin C,
kula sana matunda yenye uchachu kama Machungwa, malimao, n.k

pia Uwe unapaka asali kwenye lips mara kwa mara..
Itakusaidia sana
 
nichek upo mkoa gani nikupatie dawa 0686251188
 
Pia mafuta ya nazi kupaka midomoni inasaidia
 
Hiyo ni dalili kuwa mwili wako haupati maji ya kutosha. Kunywa maji mengi, angalau glasi nane kwa siku.

Fata pia ushauri wa kula mboga za majani na matunda kwa wingi kama ulivyoambiwa na wachangiaji wengine hapo juu.
 
Back
Top Bottom