Heshima kwenu wanajamvi, nimekuwa na tatizo la kusinzia muda wa masomo hasa yale ambayo si ya Practical, naombeni msaada kama kuna dawa ya kufukuza usingizi maana nimejaribu kahawa lakini kama inapunguza basi kidogo sana.
Kunywa maji, na uepuke kukaa sehemu yenye joto, inapowezekana vua viatu. Alafu hujitahid kunote kila kinachozungumzwa, kuuliza pamoja na kujibu maswali, cdhan kama utasinzia tena
Usishibe saana ukiwa kwenye kipindi manake shibe inachangia sana kulegea legea na kusinzia na concentration inapungua.
Panga ratiba yako vizuri uwe unakula either lisaa kabla ya kipindi au baada ya hapo, sio unashindilia ugali au supu afu unaingia class, hapo lazima ulale. Kumbuka shibe ni mwana malevya.
Pata usingizi wa kutosha.
Hakikisha hujashiba sana au huna njaa unapokuwa kwenye kipindi. Unaweza kuwa na chupa yako ukawa unakunywa funda la maji kila unapohisi kusinzia nayo inasaidia.
Kama wadau walivyosema hapo chini, usipende kukaa siti za nyuma ukiwa mbele concetration ni kubwa zaidi. Andika summary na usiwaze chochote nje ya darasa.