Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
TATIZO LA KUTAMKA "R" NA "L"
Hili tatizo la shida ya kushindwa kutofautisha kati ya "R" na "L" ni tatizo jipya.
Nyakati zetu tunasoma shule ya msingi katika miaka ya 1950 tatizo hili halikuwapo
Walimu walikuwa makini kuanzia miaka ya awali katika kunyoosha matamshi ya wanafunzi yawe ya Kiswahili au Kiingereza.
Nashangaa leo kuwasikia watu waliofika hadi chuo kikuu hawajui tofauti ya "R" na "L".
Najiuliza inawezekanaje?
Hawa wamesomeshwa na walimu gani?
Najiuliza kuwa hata huko vyuoni walikuwa wakitamka, "Plesident," badala ya "President?"
Nilipokuwa sekondari niliingia katika mchuano wa English Elocution shule za Dar-es-Salaam.
Shule yetu St. Joseph's Convent miaka yote tukishinda nafasi ya kwanza na sababu ni kuwa shule yetu ilikuwa English Medium toka enzi na enzi.
Kiingereza kilikuwa ndiyo Kiswahili chetu.
Imefika siku ya mchuano kuchagua watakaokwenda kuwakilisha shule yetu.
Kwangu haikuwa shida wala tabu kuhifadhi ukurasa mzima wa William Shakespeare.
Mwalimu wangu wa Kiingereza Mrs. Grant kasimama mbele yangu kunisikiliza.
Darasa zima liko kimya.
Nimechagua hotuba ya Dr. Martin Luther King "I Have a Dream."
Nashuka bila tabu bila kujikwaa popote.
Hifdhi nilijifunza chuoni yaani madrasa na walimu wangu wa kwanza nawakumbuka Mwalimu Badi na Mwalimu Mussa walionihifadhisha majina ya Mtume kwenda nyuma.
Yote yalikuwa yamenasa.
Nilikuwa hata darasa la kwanza sijaanza.
Hiki kilikuwa Kiarabu na ilinisaidia sana baadae katika matamshi yangu katika lugha ya Kiingereza.
Ndiyo maana niliingia kwenye mchuano bila shida wala hofu.
Sikupita mpambano huu.
Nini sababu ya kushindwa kwangu?
Mrs. Grant mwalimu wetu wa Kiingereza hakunipasisha kwa kuwa mshindani mwenzangu alikuwa na "accent" nzuri akikizungumza Kiingereza kama Mwingereza mwenyewe.
Mrs. Grant alikuwa Mwingereza.
Haikuwa tatizo la "Glound" badala ya "Ground" lililonifanye nishindwe.
Ndiyo leo nashangaa kumsikia mtangazaji wa Radio na TV akitamka, "Blitish Bloadcasting Coplation."
Maini yananikatika nikisikia matamshi hayo.
Tunatokaje katika shida na dhiki hii?