Tatizo la kutokwa na damu puani nini sababu??

Tatizo la kutokwa na damu puani nini sababu??

walikuyu

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2018
Posts
934
Reaction score
1,981
Wakuu habari za jioni,

Kama kichwa kinavyojieleza, shemeji yenu anasumbuliwa na damu kutoka puani hari hii inaanza tu wakati anaanza kupiga chafya mfululizo gafla damu zinaanza kutoka lakini baada ya muda zinatoka pia tatizo ili huwa halimtokei mara kwa mara inakaa muda sana hata miezi miwili anaweza akaona tena inatokea.

Najua humu kuna wabobezi wa mambo naomba mwenye kufahamu shida hii atoe msaada tafadhali.

Nawasilisha.
 
Inawezekana akawa na damu nyingi kupita kiasi (High Blood Count), au mishipa midogomidogo ndani ya pua imechanika...(hii inaweza kutokana na yeye kupenga mafua kwa nguvu) kupekecha sana pua (Nose picking), Kuumizwa kwa mfano kwa kugongwa na kitu kigumu au kupigwa

Zote hizo zinaweza kuwa ni sababu...lakini kwa kuweka maji ya baridi au barafu kwny paji la uso au kichwa ndani ya dakika chache mpaka nusu saa itazuia hiyo Bleeding
 
Wakuu habari za jioni, kama kichwa kinavyojieleza, shemeji yenu anasumbuliwa na damu kutoka puani hari hii inaanza tu wakati anaanza kupiga chafya mfululizo gafla damu zinaanza kutoka lakini baada ya muda zinatoka pia tatizo ili huwa halimtokei mara kwa mara inakaa muda sana hata miezi miwili anaweza akaona tena inatokea. Najua humu kuna wabobezi wa mambo naomba mwenye kufahamu shida hii atoe msaada tafadhali.
Nawasilisha.
Tiba ya hilo tatizo iko hapa
 
Mimi huwa inanitokea nikakaa juani kwa Muda Mrefu nilivyokuwa mdogo tatizo lilikuwa linajirudia Rudia kwasababu yakucheza mpira juani.

Umri unavyozidi naona tatizo linazidi kupungua. Kwa mwaka naweza kutokwa mara mbili au Tatu.

Ni miongo zaidi ya mitatu sijaona madhara yake.
 
Tiba ya hilo tatizo iko hapa
Asante sana mkuu
 
Mimi huwa inanitokea nikakaa juani kwa Muda Mrefu nilivyokuwa mdogo tatizo lilikuwa linajirudia Rudia kwasababu yakucheza mpira juani.

Umri unavyozidi naona tatizo linazidi kupungua. Kwa mwaka naweza kutokwa mara mbili au Tatu.

Ni miongo zaidi ya mitatu sijaona madhara yake.
Pole sana mkuu, natumaini litaisha kabisa ilo tatizo
 
sababu ni nyingi inawezekana kukawa na ukavu puani namaanisha makamac hamna, vidonda vdogovdogo ndani ya pua, pia magonjwa ya allergies hvyo ni vya karaka haraka ambavyo vnaweza kuchunguzika hata na wew mwenye kama vyote hapo juu kwa kukagua vko saw na shinda inaendelea soma👇

vitu vingine ni:-
  1. Magonjwa ya Mfumo wa Upumuaji wa Juu (Upper Respiratory Infections)
  2. Matatizo ya Figo na Ini
  3. Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu (cardiovascular diseases) kama hypertension
  4. Matatizo ya Kuganda kwa Damu (Coagulation Disorders)
  5. Uvutaji wa Sigara na Matumizi ya Dawa za Kulevya
  6. Magonjwa ya Neoplasia (Tumors)
  7. na hata Mabadiliko ya homoni yanaweza kuathiri mishipa ya damu, hasa kwa wanawake wakati wa ujauzito au wakati wa hedhi.
vipimo kama MRI(magnetic resonance imaging), FBP(full blood picture), au nasal endoscope kama itapatikana nau ushauri wa baada ya vipimo hivyo ndio utakua wa msingi zaidi

Atakua saw tu.
 
Asante sana kwa maelezo mazuri ngoja tutaenda kwa daktari kupata vipimo kwa uchunguzi zaidi
 
Back
Top Bottom