Kwa siku za hivi karibuni nimekuwa mtu mwenye hasira nyingi tofauti na zamani. Mtu anaweza kunikorofisha kwa jambo dogo ila mimi nikalichukulia kwa mapana sana.. Sijajua tatizo ni nini ila hiki kitu nakuta kimenitokea tu.
Je hili jambo linasababishwa na nini?
Ipi suluhu yake na kuna dawa yeyote ya kutatua tatizo hili ili hali yangu irudi kama zamani?
Msaada tafadhali.
Pole sana! Jaribu kula ndizi mbivu mara kwa mara kwa kiasi fulani inasaidia kupunguza hali uliyokuwa nayo, kwa maelezo zaidi fungua link hii
20 Minutes to Less Stress - Banannas
Kaka punguza soda na bia hasa cokes, pepsi, coca, Azam cola na nyingine za zote za ges nyingi, kunywa maji kwa wingi, nilikuwa na tatizo kama hilo ila kadri siku zinavoendal linanitoka
usisoangalie movie za kusikitisha na kuudhi. usipende kufuatilia habari za kuudhi. angalia movie za kuchekesha, katoon, stori za kufurahisha n.k.
KUMBUKA:
hasira za nyumbani usizipeleke kwenye daladala. mia