Tatizo la madoa meusi kwenye meno na tiba yake

Tatizo la madoa meusi kwenye meno na tiba yake

Dr PL

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2024
Posts
327
Reaction score
537
causes-of-black-tooth-on-tooth.jpg

Picha kwa hisani ya Google.

Madoa meusi kwenye meno ni hali ya upotevu au kutokuwepo kwa weupe wa kawaida wa meno, hivyo meno kuwa meusi au hata kahawia. Madoa meusi kwenye meno husababishwa na vitu vingi. Mfano
-Umri: kuna watu kadri wanavyozeeka hali ya muonekano wa meno hubadilika kuwa nyeusi.

-Uchafu kwenye meno ambao hutokana na upigaji mbovu wa mswaki au kutokupiga mswaki mara kwa mara. Hii husababisha uchafu kukusanyika muda mrefu na hubadilika rangi kadri muda unavyokwenda na kuwa meusi.

-Matumizi ya sigara: uvutaji wa sigara husababisha utando mweusi kwenye meno kutokana na ukungu wa moshi mweusi wa sigara au tumbaku. Pia utumiaji wa ugoro huweza husababisha hali hii kutokea.

-Matumizi ya mara kwa mara ya aina fulani za dawa na vyakula/vinywaji ambavyo vina rangi nyeusi hivyo kuacha utando mweusi.

-Kuharibika/kutoboka kwa jino/meno. Kutokana na kulika kwa sehemu ngumu ya juu ya jino (enamel) uharibifu hutokea kwa sehemu ya chini ambayo huharibika na kuwa nyeusi.

-Vinasaba (genetics): kuna baadhi ya watu ambao kwenye familia zao huzaliwa wakiwa na hali ya weusi katika meno yao.

-Madini chumvi ktk maji yanayotumiwa kila siku (fluorosis). Kuna maeneo ambapo maji yake yana madini chumvi ya aina fulani kwa wingi sana, kwa hiyo wenyeji wa maeneo hayo wanaotumia maji hayo hupata hali ya rangi ya kahawia ktk meno na wakati mwingine hubadilika kuwa nyeusi.

-Magonjwa ya mfumo wa chakula. Meno meusi pia inaweza kuashiria au kuwa dalili mojawapo ya magonjwa ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula hasa yale ambayo husababisha kulika/kutoboka kwa sehemu ngumu ya juu ya jino mfano kuna ugonjwa uitwao Celiac disease ambayo hutokana na mtu na mzio na aina fulani za nafaka (ngano, gluten).

Matibabu:
Ili kutibu hali hii ni lazima kisababishi kijulikane. Pia kuimarisha usafi wa kinywa husaidia kuzuia hali hii kutokea. Vinginevyo ni muhimu kuwaona wataalamu/madaktari wa kinywa na meno kwa ajili ya uchunguzi na matibabu sahihi ikiwa ni pamoja na kufanyiwa usafi maalumu wa kinywa na meno.
 
Back
Top Bottom