Tatizo la madonda sugu kooni

Tatizo la madonda sugu kooni

safetymaster

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2016
Posts
226
Reaction score
285
Wassalam wanajukwaa.

Afya kwa mwanadamu ni tunu kubwa ambayo kuwepo kwake kunamuwezesha (binadamu) kwa kiwango kikubwa kuwa ni mwenye furaha na utulivu kwa ujumla.Ni dhahiri kwamba mwili wa binadamu unapokosa tunu hii adhimu huwa ni wenye kuathirika katika mambo mbalimbali kama vile kimaumbile,kisaikolojia na hata kinafsi.

Wacha niende kwenye nia na madhumuni ya kilichonifanya kuandika Uzi huu.

Kifupi nina Dada yangu ambaye Mungu kamjaalia ana watoto wanne.Dada huyu kapatwa na tatizo la kuugua "madonda sugu" kooni.

Alianza kuhisi madonda mnamo Novemba 2016.Alianza kwa kuhisi kama kuna utando fulani ndani ya koo pale alipomeza mate.akaenda hospitali akamuona daktari akapatiwa dawa za madonda.Mojawapo ilikuwa ni Ampicillin na ampiclos Dawa hizo hazikufanikiwa kumsaidia.

Desemba 2016 tena akarudi hospitali nakumuelezea tena kuhusu hali yake.Akabadilishiwa dawa lakini hapakuwa na mafanikio.Alipewa amoxylin pamoja na nyustatin.

Kwa kuwa alikuwa anaweza kula na kufanya shughuli nyingine ndogondogo akaona apumzike asiende tena hospitali.

Mnamo machi 2017,haya madonda yamerudi kwa kasi.

Hapa sasa ndo akaanza kuona ni ugonjwa serious.Akarudi tena hospitali ile ile akaandikiwa sindano,lakini wapi!sindano ilikuwa ni crystalpen.

Baada ya hapo akatumia fluconas.Nazo zikashindikana.

Daktari akamuandikia dawa za vidonda vya tumbo.Lakini haikuwa!

Akaendelea kutumia dawa zingine kutokana na maelekezo ya daktari lakini hazikufanikiwa.Aliandikiwa sindano inaitwa "power safe".Sina uhakika na uandishi wa jina la hiyo sindano maana kanitamkia yeye

Katika kupambana na kutatua tatizo,akakutana na mtu baada ya kumuelezea yule mtu akamwambia anaumwa kitu kinaitwa "bawasiri" kutokana na dalili alizompa ambalo ndio limepelekea tatizo hilo.

Miongoni mwa dalili alizozielezea huyu mgonjwa ni

1.mgongo kuuma

2.Shingo pia kuuma

3.alikuwa akipata shida katika haja kubwa,alitoa haja kubwa yenye mchanganyiko na damu.

4.kinyama kilikuwa kimeota maeneo ya haja kubwa.

Baada ya kutoa maelezo hayo,Mwanzoni mwa July 2017 akawa ameelekezwa kutumia dawa za mitishamba.Baada ya kutumia dawa zile,(kile kinyama) kimeonesha kama kupotea.

Timbwili limeanza sasa hii katikati ya July, ambapo madonda yameota kwa kasi kiasi cha kuweza kuyahisi ukiweka mkono "maeneo ya koo kwa nje".Lakini sio hivyo,sasa hivi yamekuja hadi kwenye ulimi yanaonekana.

Ndugu wana jamiiforum,naamini humu wamejaa madaktari na wataalam wa afya wa uhakika.Naombeni msaada katika kutatua tatizo la huyu dada yangu.

NB:Uandishi wa majina ya dawa unaweza usiwe sahihi kwani amenitamkia mgonjwa na vilevile mie mwandishi si mtaalam wa madawa.

Nawasilisha!



Post sent using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom