Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Hali ya upatikanaji wa Maji kwa sasa kwa Mji wa Geita ni asilimia 75 kwa Wakazi wasiopungua 360,000. Mji wa Geita ni moja ya miji ambayo inakuwa kwa kasi hasa kwa shughuli za kiuchumi na Wananchi wengi wanajenga Milimani ukilinganisha na usawa wa miundombinu ya Maji ya inayohudumia na hivyo kupeleka baadhi ya wateja kupata Maji kwa mgao.
Serikali inaendelea kutekeleza Mradi wa utanuzi wa Chujio la MajiSafi eneo la Nyankaga kwa gharama ya TZS Bilioni 1.17 ambao umefikia asilimia 95. Kukamilika kwa Mradi huo mwezi Novemba 2024 kutaongeza lita milioni 11 kwa siku kutoka lita 8 kwa siku za sasa.
Aidha Serikali pia inaendelea kutekeleza Mradi mkubwa wa Maji ya Ziwa Viktoria kutoka Senga na kuleta Mjini Geita kwa gharama ya TZS Bilioni 124. Mradi huu wa Maji unatekelezwa na kampuni ya AFCONS
Mradi huu mkubwa utakuwa na uwezo wa kuzalisha lita Milioni 45 kwa siku na utanufaisha Kata zote 13 za Mji wa Geita na Vijiji 19 vya Halmshauri ya Wilaya Geita kwa asilimia 100. Wananchi wataanza kufurahia huduma ya mradi huo mwezi Oktoba, 2025.
Waziri wa Maji
Jumaa Aweso
Soma Pia: Rais Samia alivyokuja Geita tulipata maji, tangu kaondoka shida imerudi palepale