Tatizo la maumivu ya kifua

Y2k

Member
Joined
Apr 21, 2012
Posts
77
Reaction score
27
JF Doctor Naomba ushauri wako ama chochote ambacho unaweza kunieleza. Nina tatizo la kifua hapa katikati kuna maumivu fulani nayasikia mara kwa mara, nilishawahi kupiga x-ray hospital fulani wakanionesha picha na kunambia nina tatizo la Asthma na wakanieleza nina alegi na harufu na vumbi. Wakanipa dozi ya sindano na Vidonge vya kumeza nikamaliza, Baada ya muda tatizo likajirudia nikapiga tena nikaonekana sina kitu lakin mpaka natuma ujumbe huu tatizo bado lipo na pia linakuja na dalili za homa mdomo kutoka vidonda. Nikamtafuta doctor mmoja nikamueleza akaniambia tatizo la mdomo hua hata yeye linamtokea kwa hiyo ni kama common halina matatizo labda linasababishwa na mswaki kuwa mgumu akaniandikia dawa za kutumia lakini nalo huwa kila muda wa wiki kazaa linanitokea, nikamueleza labda hiki kifua naweza kuwa na tb akaniambia hapana ni maumivu tu
Naomba ushauri wako Doctor
 
ni wakati gani unapata hayo maumivu? je, huwa unashindwa kupumua? je, huwa maumivu yanaenda katika viungo vingine? je, huwa unakuwa kiuungulia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…