Habari za mwaka mpya wakuu, Kumekua na changamoto ya mawasiliano hapa nchini, kama mwaka mzima sasa, hususani kwenye mawasiliano ya kupiga/kupokea simu, kutuma/kupokea ujumbe wa maandishi, na kuperuzi kwenye mtandao wa internet, je hili suala litakua linasababishwa na nini, ni ubovu wa miundo mbinu ya mawasiliano, au ni weledi mdogo wa wafanyakazi wa idara husika au kuna jambo lingine nyuma ya pazia, kwa mfano mimi kulingana na uelewa wangu mdogo, inawezekana kuna udukuzi mkubwa unaendelea, hasahasa kipindi hiki ambacho tunaelekea kufanya maamuzi muhimu, maana kuwasiliana sasa muda mwingine imekua kero, tofauti na miaka kadhaa nyuma. nawasilisha.