Tatizo la meno kuchimbika (baina ya jino na fizi)

Globu

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2011
Posts
8,659
Reaction score
2,227
Wakuu habari za sikukuu. Nina tatizo la meno kuchimbika baina ya jino na fizi. Na sababu kubwa iliyofanya hivyo ni kupiga brush kwa muda mrefu na kutumia nguvu. Napata shida sana wakati wa kula. Kwa wataalamu wa meno msaada unahitajika.
cc MziziMkavu.
 
Last edited by a moderator:
Hatua ya kwanza acha kupiga mswaki kwa nguvu.Jaribu kutafuta miswaki yenye vifanyio laini na tumia dawa ya meno sensodyne, with time hiyo hali itakwisha. Pamoja na hayo nakushauri umwone daktari wa meno maana kama yamekwanguka sana yatahitaji kuzibwa.
 
Natumia Sensodyne, vilevile nimepunguza kutumia nguvu wakati wa kupiga mswaki ila kumbuka meno ni mazima isipokuwa yameanza kuachana baina ya fizi na meno.
 

Mkuu kuziba fizi!!!
 
Pole sana ndugu jaribu kwenda kumuona Daktari wa meno na upende kula sana machungwa na vitamin c.
 
Hata mie ninameno mengi yaliyochimbika tena yanauma hadi kichwa,shingo maumivu mtupu
 
Kumuona daktari ni Muhimu sana,lakini pia kuna dawa nzuri sana za mitishamba,nakumbuka kuna dawa nilinunua maeneo ya chelinze,ilikuwa nzuri sana kuna rafik yangu meno yake yalikuwa yanacheza cheza yote lakini alivyotumia yakarudia katika hali yake ya kawaida,sema zinapatikana kwa shida.
 

Tutajie jina kwa msaada labda huku kwetu zinapatikana
 
nakushauri muone Daktari wa meno,,1.atasaidia kujua kisababishi 2.atapendekeza tiba sahihi, pale itakapoitajika.
kwa biology yangu , hii kitu inaweza kusababishwa na Vitu vingi kama vile upungufu wa vitamin k, vitamin C, upungufu wa chembe sahani, uhaba wa protein zinazosaidia damu kuganda mwilini pale in apoitajika, maambukizi Kwenye fizi etc.Pia ukizangatia ni tatizo la muda mrefu)(zaidi ya miaka 20)uwezekano wa visabibishi vikawa Kwenye
vinasaba(genetic). nakushauri uende kwa Daktari kwa uchunguzi na ushauri,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…