Tatizo la mimba zisizotarajiwa ni kubwa kiasi gani huko Ulaya na Amerika?

Tatizo la mimba zisizotarajiwa ni kubwa kiasi gani huko Ulaya na Amerika?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Naomba kujua je huko nchi zilizoendelea na penyewe watu bado wanapeana mimba zisizotarajiwa kwa sababu tu ya kunogewa na penzi au huko walishatoka hio level na kwamba Lazima mimba ipangwe.

Huku kwetu ni kawaida mwanaume huna hili wala lile unashangaa Unaletewa Habari ya ujauzito ok nataka nijue km na huko mambele kuna hio kasumba.
 
Mimba zisizotarajiwa zipo sana, lakini ni law key kwasababu kwa wenzetu wameharalisha abortion. Ukiondoa immigrants, kwa wao wenyewe mimba wanazochoropoa ni nyingi sana kuliko wanazojifungua.
Vilevile hili swala linategemea na maeneo, kwa mfano sehemu kama Scotland, Ireland au South of Belgium kumuona binti wa miaka 16 kabeba mtoto mwenzie sio jambo la ajabu sana kwahiyo usiniambie mabinti kama hawa wamepanga kupata mimba
 
Naomba kujua je huko nchi zilizoendelea na penyewe watu bado wanapeana mimba zisizotarajiwa kwa sababu tu ya kunogewa na penzi au huko walishatoka hio level na kwamba Lazima mimba ipangwe.

Huku kwetu ni kawaida mwanaume huna hili wala lile unashangaa Unaletewa Habari ya ujauzito ok nataka nijue km na huko mambele kuna hio kasumba.
Kwa wenzetu e.g. Denmark; mahusiano yapo katika ngazi 3 1. Mahusiano ya kufahamiana tu hakuna lengo.Hapa haiwezekani kupeana mimba kwani Tendo halipo. 2. Mahusiano ya Urafiki boy / girl friend. Hapa kwa kawaida msichana huwa makini na wengi hutumia contraceptives. 3. Mahusiano ya kuishi pamoja (i) Kama mume na mke lakini bila kuzaa.(ii)Kama Mume na mke kwa majaribio e.g. mwaka 1-2. bila ndoa bila watoto (iii) Kama mume na mke bila ndoa lakini waweza kuzaa watoto na kuwalea (iv) Kuishi kama Mume na Mke wenye kiapo cha Ndoa na ikiwezekana kuzaa watoto n.k.(Hii (iv)hufanyika kwa mujibu wa Dini au Bomani/Serikali.)
Ila yote kwa yote Talaka ni nje-nje.
 
Back
Top Bottom