chwechinyong
JF-Expert Member
- Aug 2, 2011
- 223
- 105
Habari wataalamu wote humu ndani.
Mke wangu anasumbuliwa sana na tatizo tajwa hapo juu. Moyo wake umejaa maji ambayo kwa mara ya kwanza yalitolewa kwa mpira na yalikuwa mengi sana ila baada ya wiki yakaonekana kurudi ingawa si katika hali ile ya mwanzo, mara hii yakiwa ni kiasi kidogo ila si kile ambacho kinatakiwa kuwepo (kwa mujibu wa madaktari). Ameshazunguka sana na tatizo hili na mbaya zaidi madaktari hawajui chanzo cha hayo maji kujaa. Ameshatumia dawa aina mbalimbali za kukausha maji moyoni, pia za TB (walihisi huenda ikawa TB inamsumbua) yapata miaka mitatu sasa ila bado maji yanaonekana kuwepo ingawa wataalamu wanasema yanapungua kwa kiasi kidogo mnoo. Hali hii humsababishia sana maumivu mke wangu upande wake wa moyo. Tumeshaenda Regency and Muhimbili katika hangaika yetu.
Je, kuna yeyote ambae kwa namna moja au nyengine ameshawahi kukutana na mgonjwa wa namna hii na tiba yake ipoje?
Je, kuna yeyote anaefahamu hospitali yoyote (ukiachwa tajwa hapo juu) walioweza kushughulika na kuliponya taizo kama hili?
Msaada wenu ni muhimu sana kwetu.
Ahsanteni